HESLB yaongeza muda wa uombaji mikopo vyuo vikuu


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo.
Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4.
“Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema.
Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone