KAZI IMEANZA DSM: Kamanda mpya kaongea tena leo
Tunae Mkuu mpya wa Polisi kwenye kanda maalum ya kipolisi ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa ambae amechukua nafasi ya Simon Sirro ambae kwa sasa ndio Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania.
Jumla ya Majambazi wanne kati ya 6 wamejeruhiwa kwa risasi na Polisi na kukamatwa kwenye eneo la Kigogo Dar es salaam baada ya mpango wao wa kwenda kuvamia kugundulika na Polisi kuwawekea mtego, majeruhi walipelekwa Muhimbili Hospital na baadae kufariki.
Polisi Dar es salaam pia imefanya oparesheni na kuwakamata watu 193 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo wacheza kamari, utapeli, bangi na mengine…
Comments
Post a Comment