MAHAKAMANI: Agnes Masogange anayo kesi ya kujibu


Mwingine ambae alifika Mahakamani leo kuendelea kufatilia kesi yake ni Video Queen Agnes Gerald ‘masogange’ ambapo kesi yake ni kuhusu tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya.
Habari mpya ya leo kuhusu kesi hiyo ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Agnes anayo kesi ya kujibu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kujitetea.
Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na ana haki ya kujitetea.
Baada ya kuelezwa hayo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu ambapo kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017 ambapo Agnes ataanza kujitetea.

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

Sugu awashangaa wanachama wa CCM