Manji Ashindwa Kufika Mahakamani Kujitetea Kutokana na Tatizo la Kiafya
Mfanyabiashara Yusuf Manji ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 31, 2017 kujitetea katika kesi inayomkabili ya dawa za kulevya kutokana na sababu za afya.
Hayo yamesemwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis kwamba kesi hiyo inaendelea na ushahidi.
Hata hivyo, kesi hiyo haikuweza kuendelea baada ya kutolewa taarifa ya Magereza kwamba Yusuf Manji anaumwa na amepewa mapumziko ya kitanda.
Baada ya kuelezwa hayo, kesi imeahirishwa hadi September 18, 2017.
Comments
Post a Comment