Tembo wapiga kambi kata ya Mkoka, wamjeruhi mtu na kula mzao mashambani
WANANCHI wanaoishi kwenye vijiji vilivyopo katika kata ya Mkoka wilaya ya Nachingwea mkoa wa Lindi, wapo kwenye taharuki kutokana na ujio wa tembo kwenye kata hiyo. Taarifa toka idara ya maliasili ya halmashauri ya wilaya ya Nachingwea, imeeleza kuwa tembo hao wanaoendelea kuvinjari kwenye baadhi ya vijiji vilivyopo kwenye kata hiyo, licha ya kuharibu mazao kwenye baadhi ya mashamba,lakini pia wamejeruhi mtu mmoja katika kijiji cha Narungombe. Akieleza matukio hayo, ofisa wanyama pori wa Halmashauri ya Wilaya hiyo kwaniaba ya ofisa maliasili na mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri, Benjamin John, alisema tembo hao wanaokadiriwa kuwa kumi walikwenda katika kijiji cha Narungombe tarehe 21 mwezi huu, ambapo walimjeruhi mtu mmoja anaetambulika kwa jina la Said Mbujeje aliyekuwa shambani mwake akiwa anavuna mbaazi. "Nikweli tukio hilo limetokea nasisi tulikwenda huko lakini hatukuwakuta, hata hivyo tumeambiwa jana (juzi)usiku wameonekana katika kijiji cha Rweje. ...
Comments
Post a Comment