Pamoja na Umaarufu Alio nao ALIKIBA Kwa Nini Bado Maskini na Diamond Platnumz ni Mwanamuziki Tajiri?


Naombeni uzii huu usichukuliwe kiushabiki bali uchukuliwe kama haki ya kila mtu kutoa ya moyoni pasipo kuvunja sheria

Kwa mda mrefu msanii Alikiba amekuwa yupo kwenye game la mziki na amejizolea umaarufu mkubwa kwa kazi zake nzuri na kujipatia mashabiki wengi huku wengine wakimuita "KING" wa bongofleva.

Lakini pamoja na umaarufu wake alionao na mashabiki wengi aliojizolea lakini bado Alikiba ni mtu mwenye maisha ya ya chini tu ambayo hayafanani kabisa na umaarufu wake

Tukija upande wa pili wa mwanamuziki Naseeb Abdul ~Diamond Platnumz yeye si wazamani sana kwenye game kama alikiba lakini nayeye ametokea kufanya kazi nzuri na kujizolea mashabiki wengi na umaarufu lakini hajaweza kufikia record ya The king himself Alikiba

Lakini ukija kwenye maswala ya maendeleo ambayo ndio kipimo cha kazi anayofanya msanii utagundua kuwa Diamond platnumz amejizolea utajiri wa kutisha zaidi ya King himself Alikiba.

Kutokana na kazi ya mziki Diamond platnumz ameweza kujipatia utajiri mkubwa ikiwemo kuachia mijengo mingi ya maana hapa town na mengine South Africa. Diamond amefunguka zaidi kwa kuanzisha biashara zake za Chibu perfume na Diamond karanga ambazo zinafanya vizuri nzuri sokoni bila kusahau mikataba yake ya matangazo na makampuni makubwa wakati king Kiba hana biashara ya maana wala maendeleo yoyote kumzidi Naseeb


Diamond platnumz amejenga ofisi yake ya kisasa na kufungua studio yake ya wasafi records ambayo inahusika kutengeneza ngoma zote za wasafi na wasanii wengine kutoka nnje kitu ambacho Alikiba hadi leo hana ofisi wala studio yake binafsi


Diamond ameanzisha Label yake mwenyewe ya Wasafi records ambayo inawasimamia wasanii wakali kama
~Rich Mavoko
~Harmonize
~Rayvanny
~lavalava
Na mtandao wa wasafi.com ambao anauza nyimbo zake na za wasanii wengine online. Label ya wasafi imekuwa ni chanzo kikubwa cha kupiga mkwanja mrefu kwa Diamond platnumz hadi ilifika kipindi TRA wakamkadiria kodi hadi swala hilo likatinga bungeni

Huku Diamond platnumz ni msanii pekee anaeilipa kodi kubwa serikali kuliko msanii yeyote hapa tz, Akiwapiku wasanii wengi wakongwe na wapya ambao wamekuwa wakimchukia lakini wengi wao hata mlango wa TRA hawaujui nikimaanisha wanaendesha kazi zao kiujanja ujanja lakini Diamond platnumz ameonyesha mfano kwa kuilipa kodi serikali kwa kazi zake zote


Wakati upande wa pili wa Alikiba yeye bado amesainiwa na Sony music na hana label yake mwenyewe wala wasanii anaowasimamia,Na wala sina uhakika kama anailipa kodi serikali kama anavyofanya Platnumz

Ukiingia katika account zao za youtube alikiba ana followers 60,000 na Platnumz anao followers 650,000 na kupitia account zao za youtube Diamond anavuta pesa ndefu kutoka youtube kutokana na video zake nyingi anazoweka kwenye account yake na followers wengi alionao

Diamond platnumz ameweza kutoa ajira kwa
~Mameneja 2
~Madancer 5
~producer 1
~Bodyguard 1
~Photographer 1
~Mtu wa IT 1
~Mbunifu 1
~Muhasibu 1
~wasanii chini ya label yake 5
Jumla 19


Ukipiga hesabu hapo Diamond platnumz anaspend zaidi ya 100 millions kwa ajili ya kulipa mishahara tu kwa crew yake au wafanyakazi wa label yake ya wasafi kwa kila mwezi huku mshahara mkubwa ukienda kwa wasanii walio chini ya lebel yake kulingana na mikataba yao

Ukija upande wa pili wa alikiba yeye ni mwajiriwa tu wa sonny music hamlipi mtu mshahara lakini maisha yake hayafanani kabisa na misifa anayopewa na mashabiki wake Mwisho wa siku utagundua kuwa alikiba anaambulia sifa tu kutoka kwa mashabiki zake mitandaoni kakini Diamond ni real money maker nikimaanisha mashabiki wanaompaka sifa Alikiba mchana ndio hao hao Wanaomtajirisha Diamond platnumz wenyewe

Na wapo watakaokuja kusema hapa kuwa alikiba sio mtu wa show off lakini msema ukweli ni mpenzi wa mungu pesa na maisha aliyokuwa nayo Alikiba hata aizidishe mara 10 hamfikii Diamond platnumz japo watu hao hao wanampaka mafuta mwa mgongo wa chupa alikiba kwa sifa ndio hao hao wanaomtajirisha Platnumz

mziki duniani kote sasa hivi ni pesa ndio mpango mzima lakini najiuliza mziki wa alikiba ni wa kuingiza pesa kutokana na kazi nzuri au ni mziki wa sifa mbona hana maendeleo yoyote?


---------------------------------------------------------------------------------------

USHAURI WANGU KWA PLATNUMZ D

Nakuomba uachane na hili bifu ulilojiwekea na alikiba kwani sio saizi yako kabisa umemzidi kimaendeleo kwa asilimia kubwa na unafanya kazi ya kumpromote tu na sikingine

Diamond platnumz level zako ni za akina Davido yaani ilibidi uweke bifu na mtu ambaye ni saizi yako Nakusihi achana nae na wala usishindane nae kwani yeye ndio anafaidika zaidi na hili bifu na anapenda liendelee. Alikiba saizi yake ni akina Dully sykes,TID,Q CHIEF,Bobjunior ndio wa kuekeana bifu lakini sio wewe

Wewe ni boss wa label kubwa ya WCB na umetoa ajira kwa vijana wengi hivyo huwezi kulingana wala kushindana na msanii Local anayefanya kazi chini ya label asiye na brand yake anayetegemea media kumpromote, hana studio wala ofisi yani yupo yupo tu,huko ni kujiaibisha tu

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone