Rais Magufuli Asitisha Bomoa bomoa Dsm

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda WAMESITISHA
zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba (17, 000)
zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la Hifadhi ya Mazingira NEMC.
Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Mhe Paul Makonda KUZUNGUMZA na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo AMEMUELEZA Mhe Rais
Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na saba
iliyotolewa HAIKUFIKA ofisini Kwake Jambo ambalo ni tofauti na Taratibu
za Utendaji kazi wa Serikali.
Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda amesema Mhe Rais amesikitishwa na
TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba na
ametoa pole kwa Wananchi waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la
Ubomoaji, na kusisitiza kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli
HAKUCHAGULIWA kwa ajili ya KUBOMOA Nyumba za watu na kusisitiza kuwa
anataka wananchi WANAOISHI katika maeneo HALALI kuachwa mana AMEPATA
taarifa kuwa huenda ZOEZI hilo lingekwenda mbali zaidi mpaka kwa
Wananchi WASIOHUSIKA.
Comments
Post a Comment