Yemen:Idadi ya waliokufa na mafuriko yaongezeka
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali kusini mwa Yemen yamesababisha vifo mpaka kufikia watu 14 sasa.
Kwa mujibu wa habari,watoto wadogo pamoja na wanawake ni kati ya wale waliopoteza maisha katika mafuriko yaliyotokea Lahij nchini Yemen.
Barabara zimefungwa kukabiliana na mafuriko nchini humo.
Ripoti zinaonyesha kuwa mvua kubwa kama hiyo haijanyesha nchini humo kwa miaka 15 sasa.
Comments
Post a Comment