China imefungia mtandao wa WhatsApp, imezitaja na sababu



zaidi ya wiki moja sasa huduma ya mtandao ya WhatsApp imefungwa na serikali ya China ikielezwa kuwa ni kwaajili ya kuimarisha usalama kabla ya kufanyika kwa mkutano wa chama cha Kikomunisti mwezi ujao.
Imeelezwa kuwa wakati mwingine, mawasiliano hayo ya WhatsApp yamekuwa yanapatikana kupitia mtandao binafsi wa VPN ambao unasimamia mitandao ya China pekee.
Pia imeelezwa kuwa mwezi Julai viliwekwa vikwazo vya watumiaji wa mtandao huo kutuma picha hata video kwa watu wengine wa China. WhatsApp inaripotiwa kuwa huduma pekee ya mtandao iliyokubalika na serikali hiyo kuwa nchini humo.

Comments

Popular posts from this blog

Tembo wapiga kambi kata ya Mkoka, wamjeruhi mtu na kula mzao mashambani

Sugu awashangaa wanachama wa CCM

Shamsa Ford ampa somo Shilole kuhusu ndoa