Dayna Nyange afunguka kuhusu Video Vixen wanaoingia kwenye muziki


Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amezunguzia kitendo cha baadhi ya video vixen kuingia katika muziki huo.

Dayna ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’ amesema wanachotakiwa kufanya ni kupigania kile wanachoamini katika muziki ila yeye huwezi kusema ni vibaya kufanya hivyo.

“Kila mmoja ana hali yake acha wapambane ana hali zao lakini hutakiwi kusema fulani hatakiwi kuingia, muziki hauna mwenyewe, so karibuni mabishosti endeleeni kupambana na hali zenu tupate matonge halafu tuchovye maisha yaendelee,” Dayna ameiambia .

Video vixen wa Bongo ambao wameingia katika muziki ni pamoja na Gigy Money na Amber Lulu kitu ambacho kiliwahi kukosolewa vikali na msanii Baby Madaha

Comments

Popular posts from this blog

Tembo wapiga kambi kata ya Mkoka, wamjeruhi mtu na kula mzao mashambani

Sugu awashangaa wanachama wa CCM

Shamsa Ford ampa somo Shilole kuhusu ndoa