Mbao yaikomalia Simba
Timu ya soka ya Simba imesimamishwa na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika jioni hii.
Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 16 kabla ya Mbao FC kusawazisha kipindi cha pili dakika ya 46 kupitia kwa Habibu Kiyombo.
Simba walishambulia kwa kasi na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 49 kupitia kwa James Kotei. Mbao FC hawakukata tamaa na dakika ya 81 wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Boniphace Maganga na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare.
Huu ni mchezo wa kwanza raundi ya 4 ambao umewaacha Simba katika nafasi ya 2 wakiwa na alama 8 wakati Mbao FC wakisogea hadi nafasi ya 9 wakiwa na alama 4.
Comments
Post a Comment