Nikki awachana Janjaro na Young Dee
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameingilia kati ugomvi wa Dogo Janja na Young Dee na kusema kwamba wanapaswa kushindana kimuziki na siyo kushambuliana katika maisha yao binafsi kwani jambo hilo linaweza kuja kuwaletea madhara kwa baadae
Nikki wa Pili amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa kufananishwa na Young Dee kwa madai ni 'mteja wa unga' jambo ambalo lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja wake Young Dee.
"Mimi naona kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia", amesema Nikki wa Pili.
Comments
Post a Comment