Nimeona Shida ya Ikulu ni Mateso Kuwa Rais- Magufuli

Nimeona Shida ya Ikulu ni Mateso Kuwa Rais- Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt John Pombe Magufuli amesema ameona shida ya Ikulu na kwamba ni mateso kuwa Rais wa nchi na yeye amekiri kuwa  ameshuhudia mateso hayo japo aliomba nafasi hiyo ya uongozi  kwa kujaribu.

Akiwa mkoani Arusha baada ya akiwatunukia Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Rais magufuli amesema kwamba aliomba nafasi hiyo kuongoza kwa kujaribu  lakini mwishowe akasukumiziwa na sasa anaona mateso yake hivyo hana budi kutatua shida za watanzania.

"Naifahamu hii kazi nayoifanya ni ngumu, ni msalaba inahitaji kumtanguliza Mungu kweli kweli . Kwa sababu ni kujitoa sadaka lakini nimekubali kuwa sadaka kwa ajili ya watanzaniakwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi waliozoea kuwaibia watanzania" amesema

"Ninaamini inawezekana hapatatokea mwingine ambaye atajitoa hivi. Najua siku moja mtakumbuka  Hamju mateso ninayoyapata. Ni shida kuwa Rais.  ndi maana Baba wa Taifa aliwahi kyusema pale Ikulu ni mateso. Mimi nimeyaona mateso niliomba kwa kujaribu wakanisukumizia huko. Magufuli

Amesema kwa kuwa watanzania wamempa nadfasi ya kuongoza basi atawatumikia kwa uaminifu kwani hakutoa Rushwa      wala kuchangiwa hela na mafisadi kuingia ikulu ndiyo maana haogopi kutumbua na kuwahakikishia wananchi kwamba atazidi kutumbua kweli kweli
Pamoja na hayo amewatakaa wananchi waachane na mambo ya vyama kwani hayana faida kama watakuwa na njaa

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone