TEKNOLOJIA: Picha 5 za teksi ya kwanza duniani kuruka angani
September 26, 2017 Dubai imefanya
jaribio la teksi ya kwanza duniani ya ndege isio na rubani ambayo
wanaamini itatumika katika shughuli mbalimbali za usafiri.
Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu
watatu kwa wakati mmoja na kuruka kwa dakika 30 kwa spidi ya kilomita 50
kwa saa na kasi yake kubwa kabisa angani ikiwa ni kilomita 100 kwa saa
na hii ikiwa ni malengo ya mji huo wa Dubai kuwa wa kiteknolojia zaidi.
Comments
Post a Comment