Ukweli kuhusu Lipstick za Wema Sepetu kuzuiwa
Meneja wa msanii gumzo bongo Wema Sepetu, amefunguka kuhusu tetesi za
bidhaa ya lipstick ya msanii huyo 'Kiss by Wema' kuzuiwa kuingia sokoni
kutokana na ubora, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli.
Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television meneja huyo
aliyejulikana kwa jina la Happy Shame, amesema mzigo huo haupo sokoni
kwa sababu msimu wa kuingiza mzigo mpya bado, na sio kama umezuiwa na
serikali kutokana na ubora.
"Hicho kitu sijasikia wala sijatumiwa 'email' kuambiwa kwamba lipstick
zimezuiwa, hivi vitu vinaenda na msimu, muda wake ukifika tutaziachia,
kwa hiyo hakuna ukweli isipokuwa kuna baadhi ya vitu tunavikamilisha
baadaye mzigo utatoka", amesema Happy Shame.
Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba 'lipstick' hizo zimezuiwa
kuingia nchini kwa sababu hazijakidhi ubora na kwamba ndio sababu ya
kutopatikana mtaani kama ambavyo zilikuwa zikigombaniwa, jambo ambalo
limepigwa na Meneja wa Wema Sepetu.
Comments
Post a Comment