Aliyeandika mtandaoni ‘Good Morning’ kwa kiarabu akamatwa na polisi kwa uchochezi

Mwanaume mmoja mwenye asili ya Palestina amejikuta mikononi mwa polisi nchini Israel baada ya kuandika neno “Asubuhi njema’ kwa lugha ya kiarabu kwenye mtandao wa Facebook.
 Hii ndio posti iliyomponza kijana huyo aliyoiweka wiki iliyopita na tayari imeshafutwa mtandaoni
Kijana huyo ambaye jina lake limehifadhiwa amekamatwa kwa makosa baada ya mtandao wa facebook kushindwa kutafsiri kwa ufasaha neno ‘Asubuhi njema’ kwa kiarabu na kutafsiri ‘Washambulie hao’ kwa lugha ya Kiyahudi.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka polisi mjini Judea na Samaria nchini Israel zinaeleza kuwa kijana huyo ni mfanyakazi wa kampuni ya ujenzi na aliposti picha hiyo akiwa katika maeneo ya West Bank.
Polisi wameeleza kuwa baada ya kuona posti hiyo walichukua uamuzi wa kumsaka kijana huyo na kumkamata ndani ya masaa matatu ili kumuhoji kuhusu kauli yake iliyotafsiriwa kama ni ya kichochezi.
Hata hivyo masaa machache baada ya mahojiano aliachiwa huru na polisi baada ya kupata msaada kutoka kwa mtalaamu wa Lugha aliyetafsiri kwa ufasaha neno hilo la ‘Goood Morning’ kwa lugha ya kiyahudi.
Facebook imekuwa ikilaumiwa na watu wengi wanaotumia lugha mbalimbali duniani kwa kushindwa kutafsiri kwa ufasaha baadhi ya maneno kutoka kwenye lugha husika.
Kwa upande mwingine Polisi wamesema walipatwa na hofu kubwa kwa kumuona kijana mwenye asili ya Palestina akiandika ujumbe huo uliokaa kichochezi huku akiwa karibu na Tinga Tinga. Ambapo eneo hilo hilo miezi miwili iliyopita kulitokea tukio la kigaidi baada ya watu waliosadikika kuwa ni magaidi waliendesha Tinga Tinga kwenye umati wa watu na kujeruhi watu wawili.
Hadi sasa polisi nchini Israel bado haina askari wanaoujua lugha ya kiarabu pengine ndio maana walichukua uamuzi wa haraka kumkamata kijana huo.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone