Birdman kutua Tanzania


Mmiliki wa lebo ya Cash Money, Birdman amethibitisha mpango wake wa  kutua nchini mapema mwakani ikiwa ni sehemu ya ziara kwenye nchi tano za Afrika.

Rapa huyo wa  Marekani, mapema wiki hii ameandika katika akaunti yake ya Instagram kuwa atafanya ziara licha ya kutoeleza ni kwa ajili ya muziki au la!

Mkongwe huyo wa Hip Hop amesifu upendo na mapokezi makubwa wanayopata kutoka nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.

Mbali na Tanzania amezitaja nchi nne ikiwamo Nigeria, Gambia, Ghana na Kenya na kuandika “Nitatembelea kwenye nchi hizi kuanzia Februari.

Birdman ameingia katika mzozo na rapa, Lil Wayne ambaye amekuwa akimtuhumu bosi huyo kuchelewesha kutoa albamu yake “Tha Carter V”.

Bifu hilo limeendelea kuwa kubwa huku baadhi ya mastaa akiwamo Rick Ross kumtaka Birdman amlipe fedha Lil Wayne licha ya meneja huyo kuwa mbogo.

Mbali na Weezy, lebo hiyo iliyojipatia umaarufu kutokana na kuzalisha mastaa wakubwa akiwamo Drake, Nicki Minaj na Tyga.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone