Helkopta yaanguka nchini Kenya


Nakuru, Kenya. Helikopta imeanguka katika ziwa Nakuru nchini Kenya muda mfupi baada ya kuruka kutoka katika hoteli moja mjini humo.

Gazeti la Nation limemnukuu ofisa wa serikali, Joshua Omukata akithibitisha kutokea kwa ajili hiyo na kusema kulikuwa kukisubiriwa boti ya uokoaji kuelekea katika eneo la tukio.

Taarifa ambazo hata hivyo zilikuwa bado hazijadhibitiwa zilisema helkopta hiyo ilikuwa imebeba watu wanne.

Seneta wa Nakuru, Susan Kihika amesema baadhi ya timu yake inayohusika na masuala ya mawasiliano walikuwemo kwenye helikopta hiyo.

Helkopta hiyo ilikuwa imeruka kutoka Hoteli ya Jarika na baadhi ya duru za habari zinasema ilikuwa ikiruka katika usawa wa chini kabla ya kuanguka.

Ripoti zinasema helkopta hiyo baadaye ilipanga kuwachukua waandishi wa habari kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa marudio utakaofanyika Oktoba 26. Waandishi hao walikuwa kwenye hoteli hiyo wakati ndege hiyo ilipoanguka.K

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone