Hizi ndizo gharama za kuiona Yanga na Simba
Taarifa kutoka shirikisho imebainisha kuwa watazamaji watakaotaka kuketi kwenye jukwaa kuu watapaswa kulipia shilingi elfu ishirini 20000/= ili kuona mchezo huo wa watani wa Jadi.
Watazamaji watakaoketi eneo la mzunguko watalipia shilingi elfu kumi, 10000/= ili kushuhudia mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mvuto wa kipekee kutokana na aina ya wachezaji walisajiliwa msimu huu wa 2017/18.
Yanga na Simba zitaingia uwanjani zote zikiwa na alama 15, Simba ikiwa juu kwa tofauti ya mabao hivyo mshindi wa mchezo huo ana nafasi kubwa ya kuongoza ligi huku akisubiri matokeo ya Mtibwa Sugar dhidi ya Singida United.
Comments
Post a Comment