Maghorofa ya Lugumi kupigwa mnada kwa mara nyingine
Dar es Salaam.Kampuni ya Udalali ya Yono imesema itapiga mnada kwa mara ya pili nyumba za kifahari za mfanyabiashara Saidi Lugumi baada ya ule wa kwanza uliofanyika Septemba 7 kukwama.
Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo, Scholastica Kevela amewaeleza waandishi wa habari leo Jumatatu kuwa lengo la mnada huo ni kufidia Sh 14 bilioni anazodaiwa Lugumi.
"Sio kweli nyumba hizi zimedoda ila thamani halisi katika mnada wa kwanza haukufikiwa na ndio maana tunarudia tena Novemba 9," amesema Kevela.
Amesema baada ya mnada wa awali kukwama walirudi kujipanga na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewapa maelekezo mengine ikiwamo thamani ya nyumba hizo.
Soma: Wateja hawajajitokeza kununua mali za Lugumi
"Wale wanaotaka majumba haya ya Lugumi waje siku hiyo na tayari Serikali kupitia TRA imetupa maelekezo mapya hasa thamani ya majumba hayo imepanda kuliko ya awali ilivyokuwa," ameongeza
Mkurugenzi huyo amesema nyumba hizo zitakazopigwa mnada ziko Mbweni JKT nyumba mbili na nyumba moja ipo Upanga.
Comments
Post a Comment