Mke wa Dk. Slaa ahitajika katika kesi ya Lulu

Kesi ya kuua bila kukusudia inayomkabili muigizaji wa filamu bongo Elizabeth Michael, (Lulu) imeendelea leo katika mahakama kuu jijini Dar es salaam, ambapo upande wa utetezi umeshindwa kuendelea kutoa ushahidi wake kwa kukosekana shahidi mwingine

Shahidi huyo aliyetajwa kuwa ni mke wa aliyekuwa katibu mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, Bi. Jacqueline Mushumbusi ambaye yuko nje ya nchi, ushahidi wake umekataliwa kupokelewa na mahakama mpaka awepo mwenyewe au askari ambaye aliandika maelezo yake afike mahakamani kutoa ushahidi huo.

Hapo jana wakili wa mshtakiwa Peter Kibatala aliiomba mahakama iruhusu kupokelewa kwa ushahidi utakaotumwa na Bi. Mushumbusi, lakini mahakama imekataa ombi hilo ikisema upande wa utetezi hauwezi kusoma ushahidi huo na kutoa uamuzi wake wa kutaka shahidi awepo mwenyewe au askari aliyeandika ushahidi huo.

Kesi hiyo imeghailishwa mpaka kesho Oktoba 25, ambapo inatarajiwa askari aliyeandika ushahidi wa Bi. Jacquline Mushumbusi, kuwasili mahakamani hapo na kutoa ushahidi wake.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone