Rais Kenyatta uso kwa uso na Jaji Maraga


Nairobi, Kenya. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenyatta na Jaji Mkuu David Maraga jana walikuwa kivutio cha aina yake wakati walipokutana kwa mara ya kwanza na kupeana mikono tangu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Agosti 8.

Rais Kenyatta amekuwa akimkosoa Jaji Maraga kutokana na uamuzi wake wa kubatilisha matokeo hayo yaliyompa ushindi.

Lakini wawili hao walikaa katika jukwaa moja wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa na kivutio zaidi kilionekana wakati Rais Kenyatta alipoanza kuwasalimia viongozi waliokaa jukwaa kuu na hatimaye kukutana na Maraga.

Walipeana mikono huku kila mmoja wao akionyesha sura ya tabasamu. Tukio hilo liliwavutia wengi huku vyombo vya habari vikionekana kulipa uzito zaidi. Nao viongozi waliokuwa wameketi meza kuu waliwageukia wawili hao wakistaajabu kuona jinsi walivyopeana mikono.

Mara kadhaa Rais Kenyatta amekuwa akisikika akimshambulia waziwazi Jaji Maraga na kudai atashughulika naye baada ya uchaguzi wa marudio uliopangwa kufanyika Oktoba 26 kukamilika.

Katika kile kilichodhihirisha mvutano huo ulikuwa mkubwa Jaji Maraga na watendaji wake walikacha kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa bunge zilizofanywa na Rais Kenyatta.

Sherehe hizo za jana zilihudhuriwa pia na Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu. Pia, walikuwemo Makamu wa Rais William Ruto na spika wa bunge Justin Muturi.

Kambi ya Nasa inayoongozwa na Raila Odinga ambaye amesusia uchaguzi wa marudio hawakuhudhuria.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone