Haya ndio maamuzi ya Mahakama kuhusu ile kesi ya Mtoto wa Diamond na Hamisa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa mtoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond Platnumz, uamuzi huo umetolewa na hakimu baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili.
Diamond aliwasilisha pingamizi kudai kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kwa kifungu ambacho sio sahihi ambapo hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na Mawakili wanaomtetea Hamisa.
Hamisa Mobetto alifungua kesi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliomba Mahakama imuamuru Diamond Platnumz atoe matunzo ya milioni tano kila mwezi kwa mtoto waliezaa, ishu nyingine ilikua ni Hamisa kutaka Mahakama imuamuru Diamond amuombe msamaha kwa kusababisha madhara yaliyoishtua familia yake.
Kwenye kesi hiyo Diamond Platnumz kupitia Mawakili wake alipinga maombi ya kudai shilingi milioni 5 kila mwezi kwa kusema kwamba ni pesa nyingi na yeye hawezi kuimudu…….. hatujui kama Hamisa atakata rufaa au ataridhika na maamuzi haya ya Mahakama.
Comments
Post a Comment