Lukaku afufukia Timu ya Taifa, atupia mbili
Eden Hazard (kulia) akipongezana na Romelu Lukaku usiku wa jana Uwanja wa Roi Baudouin mjini Brussel, baada ya wote kufunga katika sare ya 3-3 na Mexico kwenye mchezo wa kirafiki. Hazard alifunga moja dakika ya 17 na Lukaku akafunga mawili dakika za 55 na 70, wakati mabao ya Mexico yalifungwa na Andres Guardado dakika ya 38 kwa penalti, Hirving Lozano dakika ya 56 na 60.
Comments
Post a Comment