Paul Makonda apokea tani 405 za nondo

Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  leo amepokea zaidi ya Tani 405 za Nondo kutoka kiwanda cha AM Steel and Iron Mills Ltd na Mifuko ya Saruji 500 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa LAPF kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Dar es Salaam.Nondo hizo zenye thamani ya zaidi ya Shillingi Million 150 zimetolewa kama utangulizi ambapo Kiwanda hicho kimesema kitatoa Nondo za kujenga ofisi zote 402 za Walimu.

Akipokea Nondo hizo RC Makonda  ameshukuru kiwanda hicho kwa kuunga Mkono kampeni hiyo inayolenga kurejesha heshima kwa walimu na kuwapa morali ya kufanya kazi ili kuleta matokeo chanya kwa Wanafunzi.

Wakati huohuo Mfuko wa hifadhi ya Jamii LAPF umemkabidhi RC Makonda  Kiasi cha Shillingi Million 5 kwaajili ya kununua Mifuko 500 ya Saruji ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu.

RC Makonda  amewahimiza Wananchi na wadau kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofis za walimu kupitia Saruji, Kokoto, Mchanga, Nondo Mbao, Milango, Madirisha na Bati ili kufanikisha kampeni hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kiwanda hicho Shekh Shahidi  Salim,  amesema watatoa kiasi chote cha mahitaji ya Nondo zinazohitajika kwakuwa wanatambua umuhimu wa Walimu na kaziakubwa anayoifanya RC Makonda  kwenye Mkoa wa Dar es Salaam

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone