Steve Nyerere amjia juu Polepole kuhusu Wema Sepetu

“Chama chetu sio Daladala mtu anaweza kupanda na kushuka wakati wowote, ni heri akabaki hukohuko ama akaanzie kule ambako alichukulia kadi yetu,” aliandika Polepole.
Kauli hiyo imemuibua Staa wa Filamu aliyekuwa rafiki wa karibu wa Wema kabla hajahamia Chadema, Steve Nyerere ambaye amemtolea povu Polepole na kuijibu kauli yake hiyo akiandika;
“Hiki chama hujakiunda wewe wala kukianzisha wewe, umekikuta kama tulivyokikuta wote, kina waasisi wenye uchungu nacho na wako kimya.
“Wewe ni nani ukatishe watu moyo kukitumikia kama vile ndio unakimiliki, tulia polepole chama cha wote hiki, usilete ubinafsi kwenye kutumikia na kujenga ngome, hatuhitaji wenye cement na nondo tu, acha hata mwenye jiwe lake aweke kikubwa nyumba isimame, ni mchango pia” – aliandika Steve Nyerere.

Comments
Post a Comment