Posts

Showing posts from June, 2018

Mahakama ya ICC imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa DRC

Image
June 8, 2018   Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) nchini Uholanzi imemuondolea makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa DRC   Jean Pierre Bemba. Bemba alipatikana na hatia  March, 2016  kwa makosa ya uhalifu uliotokea  Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na kuhukumiwa June 21. Bemba aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na makosa hayo ameachiliwa kufuatia rufaa iliyowasilishwa kupinga hukumu hiyo.