Mahakama ya ICC imemuachia huru aliyekuwa Makamu wa Rais wa DRC




June 8, 2018 Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) nchini Uholanzi imemuondolea makosa ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu yaliyokuwa yanamkabili aliyekuwa Makamu wa Rais wa zamani wa DRC Jean Pierre Bemba.
Bemba alipatikana na hatia March, 2016 kwa makosa ya uhalifu uliotokea  Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003 na kuhukumiwa June 21.
Bemba aliyekuwa anatumikia kifungo cha miaka 18 jela kutokana na makosa hayo ameachiliwa kufuatia rufaa iliyowasilishwa kupinga hukumu hiyo.

Comments

Popular posts from this blog

Ruby azicharukia vikali media, picha linaanzia kwa Nandy

Abiria waanzisha vurugu uwanja wa ndege

Mawasiliano Yangu na Roma Sio mazuri- Moni Centrozone