DCP Mkondya aanika kilichomtesa Dsm, akiwa kaimu kamanda
Aliyekuwa Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam,
Lucas Mkondya, amesema anaondoka katika mkoa huo huku akisema moja ya
changamoto zake ni kuwapo wanasiasa.
Hata hivyo, hakufafanua alichomaanisha anaposema wanasiasa, lakini hivi karibuni kumekuwapo maneno yanayosemwa na wananasiasa.
Mkondya aliyasema hayo leo alipokuwa akiwaaga waandishi wa habari jijini
Dar es salaam na kwamba wana siasa ndiyo changamoto kubwa huku akisema
wanaoongoza kwa kuvunja sheria.
Changamoto nyingine alizoziacha Dar es salaam ni pamoja na makosa ya
barabara na makosa mengine, pamoja na kufanikiwa kupunguza kwa kiasi
kikubwa uhalifu jijini Dar es Salaam.
Mkondya ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara na leo amegana na waandishi wa habari.
Comments
Post a Comment