Kijo-Bisimba atoa neno kuhusu wasiojulikana


Watetezi wa haki za binadamu kwa umoja wao wametaka watu wasiojulikana waweze kuchukuliwa hatua za kiusalama mara moja ili kubaini wahalifu hao wanajihusisha na vitendo vya kikatili dhidi ya watu mbalimbali nakuzuia hali hiyo isiendelee kutokea tena.

Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha Sheria na Haki za binadamu, Dkt Helen Kijo-Bisimba amesema kwamba matukio hayo kukomeshwa kutajenga amani na umoja kwa watu.

Kama hatua za kisheria na za kiusalama hazitachukuliwa kwa tukio hili la kinyama litaleta shida kwa taswira ya nchi ya Tanzania kwenye nchi zingine na kuchafua serikali. Kwani hakuna nchi duniani iliyoingia katika kadhia hizi ni zikabaki salama" Bi Kijo-Bisimba
Pamoja na hayo watetezi hao  wamemuunga mkono Rais kutokubali kunyonga baadhi ya wafungwa ambao wamehukumiwa kifo

Mbali na hayo Kituo hicho kimewataka viongozi wa dini kuchukua hatua madhubuti kukemea kwa nguvu kubwa matukio hayo kwani mwisho wa matukio haya ni kuvunjika kwa amani ya nchi. Pia amewataka viongozi  wa siasa kujadili masuala ya usalama na haswa suala la utekwaji na mashambulizi ya kinyama kwa wananchi na kutoa mapendekezo yatakayoleta suluhu ya kudumu kwa usalama wa nchi.

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR