Messi apiga hat trick, Barcelona ikiua 5-0

Gwiji wa Argentina, mshambuliaji Lionel Messi akiifungia bao la kwanza kati ya matatu Barcelona jana Uwanja wa Camp Nou ikiichapa Espanyol 5-0 katika mchezo wa La Liga. Messi alifunga dakika za 25, 36 na 66 kufikisha hat trick 38 Barcelona, wakati mabao mengine yalifungwa na Gerard Pique dakika ya 84 na Luis Suarez dakika ya 90.
Comments
Post a Comment