Neema Yazidi Kuwashukia Singida United Waongeza Mdhamini

Neema Yazidi Kuwashukia Singida United  Waongeza Mdhamini
Klabu ya soka ya Singida United imeendelea kujiimarisha kiuchumi baada ya kuongeza mdhamini atakayesimamia huduma ya maji katika timu hiyo.

Mkurugenzi wa Singida United Festo Sanga amesema wanaendelea kukusanya wadau ambao watashirikiana nao kuhakikisha wanaimarisha timu yao ili kuleta ushindani kwenye ligi na hatimaye kuondoa ufalme wa Simba na Yanga.

Singida United itapata huduma ya maji kwa misimu miwili kutoka kampuni ya Bhakresa Food Product. Kwa upande mwingine nyota wa timu hiyo Dany Usengimana amerejea kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda.

Timu hiyo iliyopanda ligi kuu msimu huu inashika nafasi ya 7 katika msimamo wa ligi kuu bara msimu 2017/18 ikiwa na alama tatu baada ya kushinda mchezo mmoja na kupoteza mmoja.

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR