Straika Nicholas Gyan Rasmi Simba

Straika Nicholas Gyan Rasmi Simba
Klabu ya Simba imefunguka na kuweka sawa kuwa straika wao mpya raia wa Ghana, Nicholas Gyan ametua nchini Tanzania na kujiunga rasmi na klabu hiyo ambayo kwa sasa ndiyo klabu inayoongoza katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara 2017/2018.

Nicholas Gyan ni kati ya wachezaji ambao walikipiga siku ya Simba Day Agosti 8, 2017 ambapo Simba SC ilicheza game ya kirafiki dhidi ya Rayon Sports kutoka Rwanda katika uwanja wa Taifa Dar es salaam ambapo Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

"Baada ya kusajiliwa na kucheza kwenye siku ya Simba Day kisha kurudi Ghana kumalizia utaratibu, Nicholas Gyan amewasili rasmi kuitumikia Simba Sc. Ikumbukwe kuwa Nicholas alikuwa mfungaji bora wa ligi ya Ghana. Karibu sana Nicholas Simba Sc" alisema taarifa ya Simba

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR