AT: Hakuna msanii anayechezwa Marekani


Msanii wa bongo fleva AT ambaye sasa yupo nchini Marekani amefunguka na kusema hakuna msanii yoyote wa Tanzania ambaye nyimbo zake zinachezwa nchini Marekani kwenye vituo vyovyote vya Radio au hata kufahamika nchini humo.

AT amesema kuwa wasanii ambao wanajigamba na kusema kuwa ngoma zao zinachezwa Marekani ni waongo na kudai wasanii wachache kutoka nchini Nigeria ndiyo ngoma zao zinasikika akiwepo Davido, Wizkid pamoja na Tiwa Savage.

Msanii huyo anasema kwa Tanzania hatuna mwakilishi nchini Marekani katika muziki na kudai kuwa kidogo mtu ambaye anafahamika huko ni Alikiba kwa kuwa alipata nafasi ya kufanya kazi na msanii mkongwe wa muziki Marekani R Kelly

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR