Watu wanne wauawa na washukiwa wa al-Shabab

Watu
wanne wameuawa na watu wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa al-Shabab katika
eneo la Hindi katika kaunti ya Lamu katika eneo la pwani nchini Kenya.
Kamishna
wa kaunti hiyo Gilbert Kitiyo ameambia BBC kwamba maafisa wakuu wa
usalama katika kaunti hiyo wanakutana na watatoa maelezo zaidi baada ya
mkutano huo.
Gazeti
la kibinafsi la Standard linasema wakazi wamejitokeza barabarani katika
mji huo kuandama kulalamikia 'kukawia' kwa maafisa wa usalama kufika
eneo la shambulio.
Kisa
hicho kimetokea siku chache baada ya watu watatu kuuawa wanamgambo
wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la al-Shabab waliposhambulia basin a
gari eneo la Nyongoro, Witu katika kaunti hiyo ya Lamu.
Gazeti la Standard linasema visa vya mashambulio vimeongezeka eneo hilo wiki za hivi karibuni.
Kamishna
wa kanda ya Pwani Nelson Marwa majuzi alitangaza kwamba maafisa wa
usalama wangeanza kuangusha mabomu katika msitu wa Boni ambapo
wanamgambo wa kundi hilo la Kiislamu wanadaiwa kujificha.
Wakazi waliokuwa wakiishi msituni na karibu na msitu huo walitakiwa kuhama.
Comments
Post a Comment