Janga la Lissu ilikuwa limpate Bulaya


Mbunge wa Bunda Mjini Ester Amos Bulaya, amesema matukio hatarishi ya kiusalama yanayowatokea baadhi ya wabunge wa CHADEMA likiwemo la Lissu na Lema, ililikuwa limkute na yeye ispokuwa aliwahi kujisalimisha polisi.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television, Ester Bulaya amesema aliwahi kufuatiliwa na gari ambao alikuwa na mashaka nalo akielekea mkoani Arusha, hali ambayo iliibua hofu kwake na dereva wake, na kwenda kujisalimisha katika kituo cha polisi cha Usa River.

Ester Bulaya amesema siku hiyo wakiwa njiani kuelekea Arusha, dereva wake akamwambia anaona kuna gari inawafuatilia, na walipowakaribia walishusha kioo upande aliokaa Ester Bulaya, na ndipo akaongeza spidi zaidi kuweza kuwatoka na kwenda kuingia polisi kutoa taarifa, na kuwapa ulinzi.

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR