Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumjia juu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai na kusema kuwa anamsikitika sana kama haoni jeshi heshima ya Bunge inavyoshuka. Zitto Kabwe amesema hayo leo kupitia mitandao yake ya kijamii baada ya Spika wa Bunge Job Ndugai kuagiza na kuwataka wabunge Zitto Kabwe pamoja na Saed Kubenea wa Ubungo kufika kwenye Kamati ya Maadili na Madaraka ya Bunge kuhojiwa kutokana na kauli zao ambazo wamezitoa hivi karibuni. Kufuatia wito huo Zitto Kabwe amesema yeye atafika kwenye kamati hiyo ya maadili na Madaraka ya Bunge kama ambavyo Spika wa Bunge Job Ndugai ameagiza na kusema kuwa spika huyo kama angeweza kujua nguvu yake wala asingehaika na wabunge ambao wanakosoa kwa staha. "Spika Ndugai anajua ninavyomheshimu kama imefikia haoni heshima ya Bunge inavyoporomoka namsikitikia. Nitakwenda Kamati ya Maadili, Ndugai amekuwa Spika wa kwanza katika historia ya nchi yetu kus...
Milango ya ustaa inazidi kufunguliwa kwa Diamond Platnumz. Msanii huyo kutoka WCB ameonekana kuanza kuwateka mastaa wakubwa Marekani. Baada ya Dj Khaled kumfollow na rapper Rick Ross kumpost hitmaker huyo wa Eneka kwenye mtandao wa Instagram, Swizz Beatz na yeye ameamua kufuata nyayo kama hizo. Swizz ameonekana katika kipande ha video akimtaja Diamond. Hata hivyo haikuishia hapo producer huyo ambaye pia ni mume wa msanii Alicia Keys ame-comment katika video hiyo ambayo Diamond ameipost katika mtandao huo. “@diamondplatnumz Bless up Kingππππππππππππ,” ameandika Beatz katika video hiyo
PGG imenusurika kupata kichapo cha kwanza katika msimu buu baada ya Edson Cavani kusawazisha katika dakika ya mwisho ya mchezo, Katika mchezo huo kikubwa ni pale ambapo mchezaji ghali zaidi duniani Neymar jr alipo onyeshwa kadi nyekundu baada ya kucheza rafu mara mbili tofauti. Kitendo hiko kimewafanya wachambuzi wengi wa soka kumkosoa Neymar kwa kusema kutokana na nidhamu ya Neymar kuwa mbovu na matukio ya utovu wa nidhamu kuwepo mara kwa mara awezi kulinganishwa na Lionel Messi ambaye hana tabia hizo wala auwezi kumbuka mara ya mwisho ni lini kupewa kadi nyekundu. Kitendo hiko kimewafanya wachambuzi wengi wa soka kumkosoa Neymar kwa kusema kutokana na nidhamu ya Neymar kuwa mbovu na matukio ya utovu wa nidhamu kuwepo mara kwa mara awezi kulinganishwa na Lionel Messi ambaye hana tabia hizo wala auwezi kumbuka mara ya mwisho ni lini kupewa kadi nyekundu Refa Ruddy Buquet akimuonyesha kadi nyekundu mshambuliaji wa Paris Saint-Germain, Neymar Ju...
Comments
Post a Comment