Wafuasi wa upinzani Kenya waandamana kushinikiza mageuzi IEBC

Wafuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya National Super Alliance (Nasa) wamejitokeza katika baadhi ya miji nchini humo kushinikiza kuondolewa kazini kwa baadhi ya maafisa wakuu wa tume ya taifa ya uchaguzi.

Maafisa wa usalama Kenya wamekuwa kishika doria karibu na jumba la Anniversary Towers zilipo afisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC) jijini Nairobi.

Muungano wa Nasa ukiongozwa na Raila Odinga umetangaza maandamano ya kila Jumatatu na Ijumaa kushinikiza kuondolewa kwa afisa mkuu mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba na maafisa wengine wakuu kwa tuhuma kwamba walihusika katika makosa yaliyochangia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 8 Agost
 Uchaguzi mpya utafanyika tarehe 26 Oktoba lakini Nasa wanasema sharti mabadiliko yafanywe kwenye tume hiyo kabla yao kukubali kushiriki katika uchaguzi huo.

Comments

Popular posts from this blog

Zitto Kabwe amjia juu Spika Job Ndugai

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

MATOKEO YA PSG DHIDI YA MARSEILLE YAMELETA TOFAUTI YA MESSI NA NEYMAR