Posts

Showing posts from November, 2017

Kubenea ahojiwa na kamati ya Bunge

Image
Kamati ya  Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, imemhoji  Mbunge wa Ubungo Mheshimiwa Saed Kubenea kwa kosa la kutoa kauli ya kudharau Bunge. Akizungumza mara baada ya kumhoji Mbunge huyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Almasi Athuman  Maige (Mb) alisema, Mheshimiwa  Kubenea amefikishwa mbele ya Kamati  hiyo kujibu tuhuma inayomkabili kutokana na kauli aliyotoa kitendo ambacho   ni kinyume na kifungu cha 26 (e) na 34 (1) (a)   ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge, Sura ya 296. Mheshimiwa Maige alisema mahojiano hayo yamefanyika  leo (jana) baada ya kuahirishwa mara mbili kutokana na Mheshimiwa Kubenea kutokua katika hali nzuri kiafya na hivyo kuomba mahojiano yaahirishwe. Mheshimiwa Maige aliongeza kuwa  baada ya kumsikiliza Mhe. Kubenea itaandaa Taarifa yake na kuiwasilisha kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai kwa hatua zaidi. “Kanuni zimeweka masharti kuwa shughuli za Kamati hii zinazofanywa ...

Lissu afanyiwa upasuaji mwingine

Image
Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), ambaye pia ni Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu amefanyiwa upasuaji wa 18. Upasuaji huo ulifanyika jana katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya ambako Lissu anaendelea na matibabu tangu Septemba 7, baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 akiwa katika makazi yake, area D mjini Dodoma. Akizungumza na Mwananchi jana kwa simu, kaka yake Lissu, Alute Mughwai alisema, “Lissu leo (jana) amefanyiwa upasuaji ambao ulianza asubuhi na umemalizika salama. Nimeambiwa muda mfupi uliopita (ilikuwa saa 9.32 alasiri wakati akizungumza na Mwananchi) kuwa ameshatoka chumba cha upasuaji.” Alute alisema, “Nimeambiwa upasuaji ulikwenda vizuri na sasa atapaswa kupumzika kama siku nne kisha ataendelea na mazoezi kama kawaida.” Ingawa Alute hakueleza huo ni upasuaji wa ngapi, Oktoba 17 mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari alisema Lissu alikuwa amefanyiwa upasuaji mara 17 ...

Profesa Kitila Mkumbo ajiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM)

Image
Profesa Kitila Mkumbo amejiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM), taarifa ya Prof. Mkumbo kujiunga CCM imetolewa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida, Martha Mlata.

Balozi aeleza alivyomsafirisha Dk Shika kijasusi kutoka Urusi

Image
Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini  Urusi wakati huo, Patrick Chokala   Dar es Salaam. Siku mbili zikiwa zimepita tangu Dk Louis Shika kuelezea siku 28 za mateso aliyoyapata nchini Urusi, aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo wakati huo, Patrick Chokala amefichua siri jinsi walivyomsafirisha kijasusi ‘bilionea huyo wa nyumba za Lugumi’ kurudi Tanzania. Balozi Chokala aliyekuwa Urusi kati ya mwaka 2002 na 2008 katika kipindi ambacho sakata la utekwaji wa Dk Shika lilijitokeza, amethibitisha kuwa ni kweli Mtanzania huyo ni daktari na kwamba ni kweli amewahi kutekwa. Dk Shika anatuhumiwa kuvuruga mnada wa majumba ya mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi uliofanywa na kampuni ya Yono baada ya kufika bei ya kuzinunua nyumba hizo tatu kwa Sh3.2 bilioni, lakini akashindwa kutimiza sharti la kulipa asilimia 25 ya fedha hizo. Kushindwa huko kulipa kulisababisha awekwe rumande katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam kwa siku sita hadi alipoachiwa kwa kujidhamin...

Lukaku afufukia Timu ya Taifa, atupia mbili

Image
Eden Hazard (kulia) akipongezana na Romelu Lukaku usiku wa jana Uwanja wa Roi Baudouin mjini Brussel, baada ya wote kufunga katika sare ya 3-3 na Mexico kwenye mchezo wa kirafiki. Hazard alifunga moja dakika ya 17 na Lukaku akafunga mawili dakika za 55 na 70, wakati mabao ya Mexico yalifungwa na Andres Guardado dakika ya 38 kwa penalti, Hirving Lozano dakika ya 56 na 60.

Haya ndio maamuzi ya Mahakama kuhusu ile kesi ya Mtoto wa Diamond na Hamisa

Image
Kesi ambayo ilifunguliwa na Hamisa Mobeto siku kadhaa baada ya kupata mtoto na Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond Platnumz. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upande wa mtoto imetupilia mbali kesi iliyofunguliwa na Hamisa Mobetto dhidi ya Diamond Platnumz, uamuzi huo umetolewa na hakimu baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili. Diamond aliwasilisha pingamizi kudai kuwa kesi hiyo ilifunguliwa kwa kifungu ambacho sio sahihi ambapo hata hivyo hoja hiyo ilipingwa na Mawakili wanaomtetea Hamisa. Hamisa Mobetto alifungua kesi hiyo ambapo pamoja na mambo mengine aliomba Mahakama imuamuru Diamond Platnumz atoe matunzo ya milioni tano kila mwezi kwa mtoto waliezaa, ishu nyingine ilikua ni Hamisa kutaka Mahakama imuamuru Diamond amuombe msamaha kwa kusababisha madhara yaliyoishtua familia yake. Kwenye kesi hiyo Diamond Platnumz kupitia Mawakili wake alipinga maombi ya kudai shilingi milioni 5 kila mwezi kwa kusema kwamba ni pesa nyingi na yeye hawezi kuimudu…….. hatujui kama Hamisa atakata ru...

Rosa Ree aachia kibao kipya baada ya kusepa The Industry

Image
Rapper wa kike kutoka Tanzania Aitwaye Rosa Ree usiku wa Jana ameendelea kuonyesha kuwa yeye ndio mkali wa Kurap kwa upande wa wadada Afrika baada ya kuachia Video kali ya wimbo wake unaitwa Dow..

Mange Kimambi Ampa Hamisa Mobetto Mbinu Kabambe za Kumshughulikia Diamond Kuhusu Kulea Mtoto Wake

Image
By Mange Kimambi "Nimepitia kidogo sheria ya matunzo ya mtoto ya Tanzania. It seems sheria hiyo ipo sawa na sheria ya Marekani . Wanaangalia kipato cha wazazi na matunzo yanatolewa kulingana na kipato cha mzazi. I think Tatizo lililoko TZ ni kwamba wanawake wengi huwa wanashindwa kuprove mahakamani kipato cha mwanaume. . Hamisa don’t take it for granted kuwa umezaaa na Diamond. Kama utashindwa kupeleka ushahidi wa kipato chake unaweza pewa matunzo ya laki kwa mwezi... So please be very careful. . . Kwanza ujue Diamond hawezi kusema kipato chake cha kweli mahakamani, you have to force him. Ila mwache kwanza aidanganye mahakama kuhusu kipato chake ndo wewe utoe ushahidi.... Je unapataje ushahidi? Ushahidi wa kwanza ni uombe mahakama ikupe order ya bank account zake zoooooote. Bank zooote unazozijua Dai anaweka pesa zake wapelekee order ya mahakama kuwa wawakilishe mahakamani statement za Diamond from 1Jan 2015 mpaka sasa hivi. . Kampuni zooote zilizoratibu show ...

Kasuku wanaotafuna nyaya za mtandao Australia

Image
Mtandao wa thamani ya mabilioni ya dola nchini Australia uko kwenye hatari kutokana na uharibifu unaosababishwa na ndege aia ya kasuku. Kampuni ya mtandao ya taifa (NBN) inasema kuwa imetumia maelfu ya dola kukarabati nyaya zilizotafunwa na kasuku. Mtandao nchini Austalia mara nyingi imekosolewa kwa kasi ya chini na kuorodheshwa nanba 50 kote duniani Kasuku atamka maneno ya mwisho ya mwanamme aliyeuwawa na mkewe NBN inakadiria kuwa huenda gharama hiyo ikapanga wakati uchunguzi zaidi ukifanywa. Inaripotiwa kuwa rangi ya nyaya hizo huenda zimevutia kasuku kuzitafuta.  

Sasa ndoto zangu zinakaribia kutimia Ulaya - Samatta

Image
  MCHEZAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amesema kwamba ndoto zake zinaelekea kutimia baada ya kuteuliwa katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika mwaka huu. Akizungumza leo, Samatta amesema kwamba amepokea kwa furaha uteuzi huo ambao unazidi kumfanya aamini juhudi zake zinamsogeza karibu na ndoto zake. “Nimeupokea kwa furaha uteuzi huu, kwani inazidi kunifanya niamini juhudi zangu zinanisogeza karibu na ndoto zangu. Nadhani wachezaji wenzangu wa Tanzania wanaweza kujifunza kitu kupitia hili,”amesema. Pamoja na hayo, Samatta anasikitika ameumia mguu jana akiichezea klabu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 0-0 na Lokeren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk. Kwa kuumia huko, Samatta amesema kuna wasiwasi asiweze kuja kujiunga na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kwa ajili ya mchezo dhidi ya Benin wiki ijayo. Nahodha huyo wa Taifa Stars amesema kwamb...

Wafuasi wa Chadema kufikishwa mahakamani kesho

Image
  Wafuasi 12 wa Chadema waliokamatwa juzi usiku Kwa kosa la kumshambulia mgombea wa udiwani wa kata ya Muriet, Francis Mbise wanatarajia kufikishwa mahakamani kesho. Wafuasi hao akiwemo Kaimu Katibu wa Chadema wilayani Arusha, Innocent Kisanyage  walishikiliwa juzi na polisi eneo la FFU Kwa Morombo wakidaiwa kumshambulia mgombea huyo sehemu mbalimbali za mwili wake. Mbali na polisi kuwashikilia wafuasi hao pia gari la matangazo linalotumika katika mikutano mbalimbali ya kampeni lilishikiliwa. Akizungumza na waandishi wa habari Leo Novemba 5 Kamanda Polisi mkoani Arusha (RPC), Charles Mkumbo amesema kwamba wafuasi hao wote 12 watafikishwa mahakamani kesho. Hata hivyo, Kamanda Mkumbo alipoulizwa kuhusu gari la matangazo lililoshikiliwa siku ya tukio hakuweza kukiri au kukataa endapo wameliachia gari hilo na kufafanua kwamba wao hawana shida na gari hilo. "Sisi tumekamata watu na hatuna shida na gari la matangazo kwani tumekamata watu au gari" amesema Mkumbo ...

Paul Makonda apokea tani 405 za nondo

Image
Dar es salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  leo amepokea zaidi ya Tani 405 za Nondo kutoka kiwanda cha AM Steel and Iron Mills Ltd na Mifuko ya Saruji 500 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya jamii wa LAPF kwaajili ya Ujenzi wa Ofisi 402 za Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari Dar es Salaam. Nondo hizo zenye thamani ya zaidi ya Shillingi Million 150 zimetolewa kama utangulizi ambapo Kiwanda hicho kimesema kitatoa Nondo za kujenga ofisi zote 402 za Walimu. Akipokea Nondo hizo RC Makonda  ameshukuru kiwanda hicho kwa kuunga Mkono kampeni hiyo inayolenga kurejesha heshima kwa walimu na kuwapa morali ya kufanya kazi ili kuleta matokeo chanya kwa Wanafunzi. Wakati huohuo Mfuko wa hifadhi ya Jamii LAPF umemkabidhi RC Makonda  Kiasi cha Shillingi Million 5 kwaajili ya kununua Mifuko 500 ya Saruji ya Ujenzi wa Ofisi za Walimu. RC Makonda  amewahimiza Wananchi na wadau kuendelea kuchangia kampeni ya ujenzi wa Ofis za walimu kupitia Saruji, Kokoto, Mcha...

CHADEMA Wajiapiza Kuchukua Jimbo la Nyalandu

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kina uhakika wa kushinda uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo la Singida Kaskazini ambalo Bunge lilitangaza jana kuwa liko wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wake kujiuzulu mapema wiki hii Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene, alipoulizwa kuhusu uchaguzi huo, alisema watamtangaza mgombea wake, baada ya Nec kutangaza kuhusu uchaguzi huo. "Tutamtangaza mgombea wetu ambaye tutamsimamisha kwenye uchaguzi huo mdogo na tunaamini tutakayemsimamisha lazima atashinda," alisema Makene. Aidha kwa upande wa Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima baada ya kuulizwa iwapo amekwishapata barua kutoka bungeni  na lini itatangaza uchaguzi mdogo wa jimbo hilo, alifunguka na kudai kuwa muda ukifika watatoa taarifa.  Kutangazwa kuwa wazi kwa jimbo hilo, sasa kunatoa fursa kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kutangaza mchakato wa kupata mrithi wa Lazaro Nyalandu ambaye alitangaza kujizulu nafasi hiyo na kujitoa uanachama wa CCM mwa...

Ngassa: Simba wasitegemee mteremko kesho

Image
Mchezaji wa Mbeya City, Mrisho Ngassa. NYOTA wa zamani wa Yanga, Azam FC na Simba ambaye sasa anacheza Mbeya City, Mrisho Ngassa, ameiambia Simba isitegemee mteremko katika mchezo wao wa kesho Jumapili. Katika mchezo huo namba 72 wa Ligi Kuu Bara, Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Sokoine kukiwa na kumbukumbu ya Simba kushinda mabao 2-0 msimu uliopita. Akizungumza na Championi Jumamosi, Ngassa alisema hawatakubali kupoteza mechi yoyote watakayoicheza nyumbani ikiwemo hii dhidi ya Simba. Ngassa alisema, wanaivaa Simba wakiwa tayari wanawafahamu wachezaji wao wote nyota wenye madhara baada ya kuwaona kwenye mechi dhidi ya Yanga. “Tunawakaribisha Simba huku Mbeya, lakini wanatakiwa kuja kwa tahadhari kubwa kwa kuwa ile Mbeya City waliyoiona kwenye mechi za nyuma siyo hii ya sasa, tumebadilika. “Mbeya City ya sasa ipo fiti na imekamilika kila sehemu kwani kila sehemu imeboreshwa na tutaingia uwanjani kwa ajili ya kuchukua pointi tatu pekee. “Ha...

Mwenyekiti wa kijiji afukuzwa kazi kwa kupiga chabo

Image
  (Picha sio ya tukio husika   Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro amemsimamisha kazi mwenyekiti wa kijiji cha Sayu, Mataifa Balekele mwenye umri wa miaka 54, kwa kulalamikiwa na wananchi kuwa na tabia ya kuwachungulia kwenye madirisha wakiwa wamelala usiku (Chabo). Taarifa za mwenyekiti huyo zilifikishwa na wanakijiji kwenye mkutano uliofanyika na kuhudhuriwa na Mkuu wa Wilaya Bi, Josephine Matiro,alipokuwa kwenye ziara yake, na kumchukulia hatua hiyo ya kumsimamisha kazi huku kukemea vikali akisema ni utovu wa maadili. Akisimulia tukio hilo Ofisa Mtendaji wa kata hiyo Denis Kimwaga amesema kuwa muhusika alikiri kufanya matukio hayo na alilipishwa faini, huku akidai ni shetani alimpitia. “Kikao hicho kiliridhia mwenyekiti huyo asimamishwe kazi kutokana na tabia hiyo ya kuchungulia kwenye kaya za watu wakiwa wamelala huku yeye mwenyewe akikiri kufanya vitendo hivyo akidai kuwa amepitiwa tu na shetani na kuomba kuwalipa fedha kama fidia watu alio...