IEBC: Matokeo ya urais yatatangazwa saa tisa unusu
Naibu mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Kenya Consolata Nkatha Maina amesema matokeo ya urais kutoka maeneo ambayo uchaguzi wa marudio ulifanyika yatatangzwa saa tisa unusu alasiri. Amesema wagombea wote wa urais wamealikwa kwa shughuli hiyo. Bi Maina amesema maeneo ambayo uchaguzi haukufanyika hayawezi kuathiri matokeo ya jumla ya uchaguzi huo.