Posts

Showing posts from September, 2017

Diamondi Azidi Kuwateka Mastaa Wakubwa Kutoka Marekani

Image
Milango ya ustaa inazidi kufunguliwa kwa Diamond Platnumz. Msanii huyo kutoka WCB ameonekana kuanza kuwateka mastaa wakubwa Marekani. Baada ya Dj Khaled kumfollow na rapper Rick Ross kumpost hitmaker huyo wa Eneka kwenye mtandao wa Instagram, Swizz Beatz na yeye ameamua kufuata nyayo kama hizo. Swizz ameonekana katika kipande ha video akimtaja Diamond. Hata hivyo haikuishia hapo producer huyo ambaye pia ni mume wa msanii Alicia Keys ame-comment katika video hiyo ambayo Diamond ameipost katika mtandao huo. “@diamondplatnumz Bless up King😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂,” ameandika Beatz katika video hiyo

KESI YA AVEVA & KABURU! Jalada bado lipo kwa DPP, yapigwa kalenda

Image
Jumatano September 27, 2017, Upande wa Mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi ya utakatishaji fedha na kughushi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ bado lipo kwa DPP. Wakili wa Serikali, Vitalis Peter amemweleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kesi hiyo imeitishwa kwa ajili ya kutajwa lakini jalada la kesi bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP). Aidha, amedai kuwa DPP ataangalia kama ameridhishwa na kesi hiyo ama ala, ambapo watasubiri kama uchunguzi umekamilika. Baada ya kuelezwa hayo, Wakili wa utetezi, Evidius Mtawala kwa sababu ya taratibu zinazoendelea ni za kiofisi wanatumai jalada litaharakishwa. Kutokana na hatua hiyo Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi October 4, 2017. Evans Aveva na makamu wake, Geofrey wanakabiliwa na mashtaka matano ya kughushi, kuwasilisha nyaraka ya uongo na kutakatisha Dola za kimarekani 300,000.

Lema , Nassari Washukuru Kuitwa na Mkurugenzi wa Takukuru

Image
Wabunge wa Chadema, Godbless Lema na Joshua Nassari wamesema watapeleka kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) ushahidi kuhusu madiwani saba waliojiuzulu katika majimbo yao wanaowatuhumu kupokea rushwa ili kujiuzulu nafasi zao. Lema ambaye ni mbunge wa Arusha Mjini, amesema leo Jumatano kuwa, wanashukuru Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Valentino Mlowola kuwakaribisha kupeleka ushahidi.  "Tunashukuru sana mkurugenzi mkuu wa Takukuru kutukaribisha, tutapeleka ushahidi wetu ofisini kwake na tunaamini atafanyia kazi tuhuma hizi," amesema. Amesema mbunge mwenzake wa Arumeru Mashariki, Nassari ambaye madiwani watano katika jimbo lake wamejiuzulu amekwenda Nairobi nchini Kenya kuonana na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kupata baraka zake kabla ya kwenda Takukuru. "Nassari amekwenda Nairobi kuonana na Mwenyekiti Mbowe ili kumweleza tukio hili na akirudi tutakwenda naye moja kwa moja kwa Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Mlowola," amese...

Nikki awachana Janjaro na Young Dee

Image
Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili ameingilia kati ugomvi wa Dogo Janja na Young Dee na kusema kwamba wanapaswa kushindana kimuziki na siyo kushambuliana katika maisha yao binafsi kwani jambo hilo linaweza kuja kuwaletea madhara kwa baadae Nikki wa Pili amesema hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kupita siku kadhaa tokea Dogo Janja kutoa kauli yake ya kukataa kufananishwa na Young Dee kwa madai ni 'mteja wa unga' jambo ambalo lilizua makelele mengi kwa mashabiki wa wasanii hao pamoja na meneja wake Young Dee. "Mimi naona kuna tatizo hapo, kwa sababu wameanza kuhusisha maisha yao binafsi, kwa hiyo ningefurahi kuona wanashindana kimuziki zaidi. Maana unapokuwa maarufu ukiongea kitu ujue kinaishi kwa kipindi kirefu na hakiwezi kufutika kiurahisi, kwa hiyo ni vizuri kuchagua maneno ya kutumia", amesema Nikki wa Pili.

Kubenea aitaka Serikali kulifungulia gazeti la Mwana Halisi ndani siku mbili

Image
WahaririI wa Gazeti la MwanaHalisi linalomilikiwa na Mbunge, Saed Kubenea lililofungiwa na serikali wamekanusha taarifa ya serikali kuwa gazeti hilo linaandika habari za uongo, wamedai kuwa wao hawajawahi kuandika uongo na badala yake huandika habari kwa weledi na ukweli. Hayo wameyasema leo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na wanahabari baada ya gazeti lao kufungiwa kwa muda wa miezi 24 (miaka miwili). Aidha mmiliki wa Gazeti hilo, Saed Kubenea amesema kampuni yake Hali Halisi Publishers, imeiandikia barua Wizara ya Habari wakiitaka serikali kulifungulia Gazeti lao la MwanaHalisi ndani ya siku mbili (jana na leo), vinginevyo wataenda mahakamani kuidai serikali fidia ya Tsh. 141 Milioni kwa kila toleo.

Miili iliyokutwa eneo la bahari Coco Beach haijulikani ilikotoka - MAMBOSASA

Image
KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema miili ya wanaume watatu iliyokutwa pembezoni mwa Bahari ya Hindi eneo la Coco Beach hawajui imetoka wapi hivyo wanaendelea na uchunguzi kubaini ilipotoka. Mambosasa amesema jeshi la polisi linaendelea kupeleleza ili kujua miili hiyo imetokea mkoa upi, nchi gani na wajulikane watu hao ni wakina nani. “Miili hiyo haieleweki inatoka wapi na watu wenyewe hawajulikani kama wanatoka Tanzania, Msumbiji au Angola hivyo tunaendelea kuichunguza,” amesema Mambosasa. Maiti za watu ziliokotwa juzi katika eneo hilo mbili zilifungwa kwenye viroba huku nyingine imekutwa na jiwe kubwa lililofungwa na kamba.

China imefungia mtandao wa WhatsApp, imezitaja na sababu

Image
zaidi ya wiki moja sasa huduma ya mtandao ya WhatsApp imefungwa na serikali ya China ikielezwa kuwa ni kwaajili ya kuimarisha usalama kabla ya kufanyika kwa mkutano wa chama cha Kikomunisti mwezi ujao. Imeelezwa kuwa wakati mwingine, mawasiliano hayo ya WhatsApp yamekuwa yanapatikana kupitia mtandao binafsi wa VPN ambao unasimamia mitandao ya China pekee. Pia imeelezwa kuwa mwezi Julai viliwekwa vikwazo vya watumiaji wa mtandao huo kutuma picha hata video kwa watu wengine wa China. WhatsApp inaripotiwa kuwa huduma pekee ya mtandao iliyokubalika na serikali hiyo kuwa nchini humo.

TEKNOLOJIA: Picha 5 za teksi ya kwanza duniani kuruka angani

Image
    September 26, 2017 Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza duniani ya ndege isio na rubani ambayo wanaamini itatumika katika shughuli mbalimbali za usafiri. Ndege hiyo ina uwezo wa kubeba watu watatu kwa wakati mmoja na kuruka kwa dakika 30 kwa spidi ya kilomita 50 kwa saa na kasi yake kubwa kabisa angani ikiwa ni kilomita 100 kwa saa na hii ikiwa ni malengo ya mji huo wa Dubai kuwa wa kiteknolojia zaidi.    

Wachina wasepa na ngoma za Mrisho Mpoto

Image
Ngoma ambazo zilikuwa zinatumiwa na msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto katika maonyesha ya Utalii Duniani yaliyofanyikia nchini China zimegombaniwa na baadhi ya wachina waliojitokeza katika maonyesho hayo.  Mpoto amesema ngoma hizo ziliwavutia wadau wengi ambao walijitokeza katika maonyesha hayo kutokana na namna ambavyo zilikuwa zinapigwa.  Pia muimbaji huyo katika maonyesho hayo alipata fursa ya kutoa elimu kwa wachina hao kuhusu utalii wa ndani.

Mbunge Peter Msigwa anashikiliwa na Polisi

Image
Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, ameandika hivi;-   "Msigwa amekamatwa na Polisi huko Iringa na kushushwa kwa nguvu jukwani  ktk Mkutano halali. Msiogope baada ya giza nene asubuhi hutokea!" Taarifa hiyo iemethibitishwa na kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa Kamishna wa polisi Julius Mjengi, Ambapo ameuleza mtandao huu kuwa Msigwa alikuwa na mkutano wa hadhara leo Septemba 24, katika eneo la Mlandege mkoani humo ambapo anadaiwa kutumia lugha na matamshi ya uchochezi katika hotuba yake.  

Hudda Ampa Makavu Diamond Sakata la Kuzaa Nje ya Ndoa

Image
Diamond Platnumz ni kama centre ya ubuyu Bongo. Mrembo wa Kenya Huddah Monroe ameonekana kuwa upande wa adui yake Zari The Bosslady katika sakata zito la Diamod kuzaa na Hamisa Mobetto. Baada ya bosi huyo wa WCB kuonekana kuishinda kwa asilimia kubwa vita ya usaliti kwa kuzaa nje, kupitia mtandao wa Snapchat, Huddah ameamua kumshushia maneno mazito msanii huyo. Haya ndio maneno aliyoandika Huddah kwenye mtandao huo.

Hospitali Aliyolazwa Lissu Yapokea Fedha Kutoka Tanzania Bila Kupewa Maelezo

Image
Ofisa Kitengo cha Habari na Itikadi wa Chadema, Hemed Ali amesema Hospitali na Nairobi nchini Kenya imethibitisha kupokea fedha kutoka Tanzania lakini zikiwa hazina maelezo. Jana ofisi ya Bunge ilitoa taarifa kuelezea mchakato wa utumaji wa fedha hizo kiasi cha Sh 43 milioni ikisema kuwa zilitumwa tangu Agosti 20. Ofisi hiyo ilikuwa ikifafanua taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyewaambia waandishi wa habari kuwa alikuwa hajapa mchango huo wa wabunge. Ali aliyepo Nairobi amesema amethibitishiwa na Hospitali ya Nairobi kupokea fedha hizo kutoka Tanzania ingawa kulikuwa hakuna maelezo zaidi. “Wamenieleza kuna fedha zimeingizwa kutoka Tanzania ila hazina maelezo ndiyo wanafuatilia benki,” amesema ofisa huyo.

Nimeona Shida ya Ikulu ni Mateso Kuwa Rais- Magufuli

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt John Pombe Magufuli amesema ameona shida ya Ikulu na kwamba ni mateso kuwa Rais wa nchi na yeye amekiri kuwa  ameshuhudia mateso hayo japo aliomba nafasi hiyo ya uongozi  kwa kujaribu. Akiwa mkoani Arusha baada ya akiwatunukia Kamisheni Maafisa wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), Rais magufuli amesema kwamba aliomba nafasi hiyo kuongoza kwa kujaribu  lakini mwishowe akasukumiziwa na sasa anaona mateso yake hivyo hana budi kutatua shida za watanzania. "Naifahamu hii kazi nayoifanya ni ngumu, ni msalaba inahitaji kumtanguliza Mungu kweli kweli . Kwa sababu ni kujitoa sadaka lakini nimekubali kuwa sadaka kwa ajili ya watanzaniakwa ajili ya kuwanyoosha mafisadi waliozoea kuwaibia watanzania" amesema "Ninaamini inawezekana hapatatokea mwingine ambaye atajitoa hivi. Najua siku moja mtakumbuka  Hamju mateso ninayoyapata. Ni shida kuwa Rais.  ndi maana Baba wa Taifa aliwahi kyusema pale Ikulu ni mateso. Mimi nimey...

Haya Hapa Mjina ya Wachezaji Watakaounda Kikosi Kipya cha Taifa Stars

Image
KOCHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ametangaza majina ya kikosi cha wachezaji watakaounda kikosi hicho kipya. Kwa asilimia kubwa hakuna mabadiliko isipokuwa kipa Peter Manyika wa Singida United ameitwa kikosini hapo kuchukua nafasi ya Said Mohamed Nduda wa Simba ambaye kwa sasa ni majeruhi. Manyika ni kipa wa zamani wa Simba ambaye aliondoka kikosini hapo baada ya kukosa nafasi na kudaiwa kuwa kiwango chake kilishuka. Timu hiyo imeitwa kujiandaa na mechi ya kirafiki iliyopo katika kalenda ya Fifa ambapo watacheza dhidi ya Malawi mnamo Oktoba 11, mwaka huu. Kikosi kamili kilichoitwa na kocha huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar ni hiki hapa: Makipa Aishi Manula Peter Manyika Ramadhani Kabwili Mabeki Bonifas Maganga Abdi Banda Gadiel Michael Salim Mbonde Erasto Nyoni Adeyuni Salehe Arned Viungo Himid Mao Hamis Abdallah Mazamiru Yassin Raphael Daud Simon Msuva Shiza Kichuya Ibrahim Ajibu Morel Ergenes Abdul Hilal Hasan Washambuliaji ...

Rais Kenyatta: Uamuzi wa Kufuta Matokeo ya Uchaguzi ni 'Mapinduzi ya Mahakama'

Image
  Rais wa kenya Uhuru Kenyatta ameutaja uamuzi wa kufutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais kuwa ''mapinduzi ya mahakama''. Viongozi hao wawili walikuwa wakijibu uamuzi kamili wa mahakama ambapo majaji wa mahakama ya juu walitoa sababu zao kwa nini walifutilia mbali matokeo hayo ya urais. Idadi kubwa ya majaji hao walisema kuwa matokeo hayo hayakuwa na 'uwazi wala kuhakikiwa'. Viongozi hao wawili hatahivyo waliangazia uamuzi wa majaji wawili waliopinga uamuzi hao ambao walisema kuwa kesi iliowasilishwa katika mahakama hiyo haikuwa na uzito wowote. Rais Kenyatta alisema kuwa hakuna uchaguzi usikumbwa na makosa madogo madogo.

Ebitoke Alizwa na Penzi la Ben Pol Aomba Msaada

Image
Mchekeshaji maarufu bongo Ebitoke alizwa na kitendo cha anayedaiwa kuwa mpenzi wake Ben Pol kutopokea simu wala kujibu meseji zake, na kuomba msaada kwa watu kumuuliza msanii huyo kwa nini anafanya hivyo, licha ya kuwa na mipango mingi ya baadae. Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Ebitoke amesema kitendo hicho kinamuweka njia panda, hivyo anashindwa kujua kama anampenda kweli au alikuwa anachezea moyo wake.

Yametimia Nyimbo ya Zilipendwa Yaipiku Seduce Me ya Ali Kiba Kwa Kutazamwa na Wetu Wengi

Image
Yametimia ZILIPENDWA yaigaragaza SEDUCE ME ya Ali Kiba... . . Hiii ni baada ya Mange Kuhamisha Amsha Amsha yake Kwenye Michango ya Tundu Lissu..... . . TEAM DIAMOND SEMA *Oyoooo*

Zitto Kabwe ajitetea kwa hoja 10 mbele ya kamati

Image
Maelezo ya ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto (Mb), mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge. Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati, Mnano tarehe 13 Septemba, 2017 nilipata wito wa kufika mbele ya Kamati yako kutoa ushahidi wa masuala mbalimbali. Nilipata wito husika saa nane na dakika 40 mchana, nikitakiwa kufika mbele ya kamati yako, hapa Dodoma saa saba mchana siku hiyo hiyo. Nililetewa wito huo na RCO Mkoa wa Kigoma nikiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kigoma Ujiji. Sikuweza kufika, isingewezekana katika mazingira hayo niwe na uwezo wa kusafiri kutoka Kigoma na kufika mbele ya kamati yako hapa Dodoma. Kwanza muda ulishapita, lakini hata taratibu za kiusafiri pamoja na umbali kati ya Kigoma na Dodoma hazikuwezesha Jambo hilo. Siku iliyofuata nilipata ajali, ambapo nyumba yangu iliwaka moto wakati nikiwa njiani kwenda Nairobi kumuona mbunge mwenzetu mgonjwa, ndugu Tundu Lissu. Jana tarehe Septemba 20, 2017 nikiwa natokea Kigoma ili k...

Mbao yaikomalia Simba

Image
Timu ya soka ya Simba imesimamishwa na Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba baada ya kulazimishwa sare ya 2-2 kwenye mchezo wa ligi kuu uliomalizika jioni hii. Simba ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa Shiza Kichuya dakika ya 16 kabla ya Mbao FC kusawazisha kipindi cha pili dakika ya 46 kupitia kwa Habibu Kiyombo. Simba walishambulia kwa kasi na kufanikiwa kuongeza bao la pili dakika ya 49 kupitia kwa James Kotei. Mbao FC hawakukata tamaa na dakika ya 81 wakafanikiwa kusawazisha kupitia kwa Boniphace Maganga na kufanya mchezo huo umalizike kwa sare. Huu ni mchezo wa kwanza raundi ya 4 ambao umewaacha Simba katika nafasi ya 2 wakiwa na alama 8 wakati Mbao FC wakisogea hadi nafasi ya 9 wakiwa na alama 4.

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Kenya: Mahakama ya Juu yaiumbua Tume ya Taifa ya Uchaguzi

Image
Mahakama ya Juu imeitupia lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kwa kusababisha kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika Agosti 8, mwaka huu. Katika maelezo ya kina kuhusu sababu za matokeo hayo kufutwa Septemba Mosi, Naibu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alifichua namna IEBC ilivyoudhi na kukaidi maelekezo iliyopewa na Mahakama ya Juu kufungua kompyuta ili kuthibitisha mfumo wa kuhifadhi takwimu baada ya upinzani kulalamika kwamba ulidukuliwa. Mwilu alisema mfumo wa Tehama wa IEBC uliingiliwa na ukachezewa na takwimu zilizomo zikabadilishwa. "Mfumo mzima umechezewa na umechafuliwa au IEBC iliingilia takwimu na ilikana kuwa mfumo wake uliingiliwa," alisema. "Amri tuliyotoa ufanyike uchunguzi ilikuwa fursa pekee adhimu kwa IEBC kuwathibitisha uongo wa waliofungua kesi lakini IEBC haikutii amri ya mahakama.” Mwilu aliongeza kwamba tume hiyo "mara kwa mara" haikutii amri hali aliyosema ilifikia “kiwango cha juu". "IEBC ili...

Zari Azidi Kutoa Povu Ajiliwaza na Mkwanja Wake Uliojaa Banki

Image
Kufuatia sakata la mzazi mwenziye kuchepuka na kuzaa na mwanamitindo maarufu Bongo, mwanamke shupavu na mjasiriamali, Zarinah Hassan ‘The Boss Lady’, amesema hakuna cha kumliza juu ya sakata hilo kwani akaunti yake benki imejaa mkwanja wa kutosha. Zari alitoa povu kwenye komenti aliyomjibu shabiki wake ambaye alikuwa akimuonea huruma na kusema kwamba anajua kuwa ameumizwa sana na kitendo hicho cha ‘Baby’ wake kuzaa na Hamisa Mobetto, sema tu analilia kwa ndani. Mpaka saa Zari bado hajaweka wazi kuwa ataendelea na mzazi mwenziye huyo ambaye ni mwanamuziki wa Bongo Fleva, au atachukua hatua gani, ikiwa ni siku moja tu imepita tangu mzazi mwenziye huyo akiri hadharani kuwa mtoto wa Mobetto ni wake.

Alichokiandika Zari baada ya Diamond kumsalit

Image
Zari Aamka Asubuhi Hii na Kuandika Ujumbe Huu Kuhusu Kuchitiwa na Diamond . #Zari Am such an early morning person as some can see on my snap, usually up by 5am. Let's start this day on a different note, shall we🤗 Ladies and gentlemen I've heard you loud and clear, the advises, the consolation, the pity, the hurt you feeling on my behalf most of all the betrayal. But let's look at this on the positive side. When a person chooses to cheat on you it's not YOU actually its THEM which usually turns out that they played themselves while they thought they are playing you. You should never look down on yourself, don't ever think you are worthless because of another person's mistake & never blame yourself. But always look at how to pick yourself up and get going. That said, with my birthday approaching let's put all this negative energy behind us and appreciate, LIFE! 🌹 

Polisi Dar yakamata ‘Wasiojulikana’ watano

Image
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limetangaza kuwakamata watu watano ambao wamekiri kufanya uhalifu na kuvunja katika ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys iliyopo katika jengo la Prime house, Mtaa wa Tambaza, Upanga jijini Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi limeweza kuwakamata watu hao ambao mwanzo baadhi ya wananchi walikuwa wakisema watu wasiojulikana ambao walifanya uhalifu huo na kudai wamekiri kuhusika na uvunjaji wa ofisi hiyo na kuiba. "Kutokana na msako mkali jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano kuhusiana na kesi ya uvunjaji wa ofisi ya Mawakili ya Prime Atorneys mnamo Septemba 12, 2017 jeshi la polisi lilipokea taarifa ya kuvunjwa kwa ofisi ya mawakili hao ambapo wahalifu hao walifanikiwa kuvunja na kuiba kasiki iliyokuwa na pesa milioni tatu laki saba, waliiba kompyuta mpakato mbili pamoja na nyaraka mbalimbali za ofisi hiyo na wateja...

Baada ya Diamond kufunguka, RC Makonda kamwandikia Zari

Image
Baada ya Diamond Platnumz kuweka wazi kuwa amezaa mtoto na Hamisa Mobetto akiwa kwenye mahojiano na Leo Tena ya Clouds FM leo September 19, 2017 kisha Zari kumuonya kuwa asimjaribu ishu hiyo sasa imefika hadi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda. RC Makonda ameandika kwenye Instagram yake akimwambia Zari kuwa ana uwezo mkubwa wa kupita kwenye dhoruba na akaendelea kubaki imara na kuendelea kupata heshima kutoka kwa familia yake. RC Makonda kaandika >>>”Thamani yako kwangu bado ni kubwa sana, kwani uwezo wako wa kupita kwenye dhoruba na ukabaki imara na familia yako unaendelea kukupa heshima.”  

Rick Ross amempost tena Diamond Platnumz

Image
Diamond ni balozi wa kinywaji hicho cha Belere na yeye amekua Staa wa pili kutoka Afrika kupostiwa na Rick Ross baada ya siku kadhaa zilizopita mwanadada kutoka nchini Kenya Huddah Monroe pia kupata bahati hiyo ya kupostiwa na Staa huyu wa Hollywood. Ikiwa zimepita siku nane toka rapa maarufu wa Marekani Rick Ross ampost Staa wa Bongp Diamond Platnumz katika ukurasa wake wa Instagram  kwa mara ya kwanza akiwa amebeba chupa za kinywaji cha Belere ikiwa ni ishara ya kukinadi kinywaji hicho, usiku wa September 17 amempost tena.  

Ukweli kuhusu Lipstick za Wema Sepetu kuzuiwa

Image
Meneja wa msanii gumzo bongo Wema Sepetu, amefunguka kuhusu tetesi za bidhaa ya lipstick ya msanii huyo 'Kiss by Wema' kuzuiwa kuingia sokoni kutokana na ubora, na kusema kwamba taarifa hizo hazina ukweli. Akizungumza na mwandishi wa habari wa East Africa Television meneja huyo aliyejulikana kwa jina la Happy Shame, amesema mzigo huo haupo sokoni kwa sababu msimu wa kuingiza mzigo mpya bado, na sio kama umezuiwa na serikali kutokana na ubora. "Hicho kitu sijasikia wala sijatumiwa 'email' kuambiwa kwamba lipstick zimezuiwa, hivi vitu vinaenda na msimu, muda wake ukifika tutaziachia, kwa hiyo hakuna ukweli isipokuwa kuna baadhi ya vitu tunavikamilisha baadaye mzigo utatoka", amesema Happy Shame. Hivi karibuni kumekuwa na tetesi kwamba 'lipstick' hizo zimezuiwa kuingia nchini kwa sababu hazijakidhi ubora na kwamba ndio sababu ya kutopatikana mtaani kama ambavyo zilikuwa zikigombaniwa, jambo ambalo limepigwa na Meneja wa Wema Sepet...

Dayna Nyange afunguka kuhusu Video Vixen wanaoingia kwenye muziki

Image
Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amezunguzia kitendo cha baadhi ya video vixen kuingia katika muziki huo. Dayna ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Chovya’ amesema wanachotakiwa kufanya ni kupigania kile wanachoamini katika muziki ila yeye huwezi kusema ni vibaya kufanya hivyo. “Kila mmoja ana hali yake acha wapambane ana hali zao lakini hutakiwi kusema fulani hatakiwi kuingia, muziki hauna mwenyewe, so karibuni mabishosti endeleeni kupambana na hali zenu tupate matonge halafu tuchovye maisha yaendelee,” Dayna ameiambia . Video vixen wa Bongo ambao wameingia katika muziki ni pamoja na Gigy Money na Amber Lulu kitu ambacho kiliwahi kukosolewa vikali na msanii Baby Madaha

Kocha wa Singida United Pluijm amaliza kifungo chake

Image
Kocha Mkuu wa Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, sasa yupo huru kuanza kukaa katika benchi la timu hiyo kutokana na kumaliza adhabu yake ya kukosa mechi tatu za Ligi Kuu Bara. Pluijm ambaye msimu uliopita alikuwa kocha wa Yanga kabla ya kupewa cheo cha ukurugenzi wa benchi la ufundi klabuni hapo, alipewa adhabu hiyo Novemba, mwaka jana kutokana na kudaiwa kuwafanyia fujo waamuzi waliochezesha mechi ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting. Mholanzi huyo amemaliza kifungo chake katika mchezo wa juzi ambao Singida iliifunga Stand United bao 1-0 ugenini. Mholanzi huyo baada ya kutoka kifungoni, amesema anachokifanya kwa sasa ni kuitengeneza zaidi timu yake iweze kupambana na timu nyingine kama Simba na Yanga kutokana na wachezaji wake wengi kutokuwa na uzoefu na michuano ya Ligi Kuu Bara. “Nashukuru nimemaliza adhabu yangu na nitaanza kukaa katika benchi kwenye mechi yetu dhidi ya Kagera Sugar, kwa ufupi kikosi changu hakijaanza vibaya msimu huu japo wachezaji wangu ...

Sina Ninachokikosa Baada ya Kundi Kuvunjika na Wala Sitoshuka Kimuziki- Aslay

Image
Mwanamuziki wa Bongo Fleva anayeongoza kwa kupachikwa majina mbalimbali na kufananishwa na wasanii wakubwa kimataifa akiwemo Chris Brown, Aslay Isihaka ‘Fundi’, amesema kuwa baada ya kundi lao la Yamoto Band kuvunjika, yeye anaendelea vizuri na kazi zake wala hamna anachokikosa kwa sababu wakati anaanza hakuwa na kundi. Aslay ambaye kwa sasa anatamba na ngoma zisizohesabika kama vile, Likizo, Baby, Pusha, Nyakunyaku, Mhudumu na nyingine nyingi, alisema kuwa: “Nilianza muziki nikiwa peke yangu na nilikuwa mdogo kiumri, enzi zile za ‘Naenda Kusema kwa Mama’, ila niliweza kufanya vizuri, kwa hiyo kuingia kwenye kundi na kutoka sioni kama nitashindwa kuendeleza muziki wangu. “Kwa sababu naona ni kama zamani tu, ndiyo maana nafanya vizuri, naachia ngoma kila kukicha, na ngoma zangu kali na zinapendwa, mashabiki hawawezi kuzichoka kwa sababu mimi ni mwanamuziki mzuri, najua nini ninachokifanya, na sitegemei kushuka kimuziki.” Aslay ni mmoja kati ya wanamuziki waliokuwa wak...

Nyalandu Azidi Kukomalia Uhai wa Lissu Azidi Kuhamasisha Watu Kuchangia Gharama za Matibabu

Image
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu (CCM) amendelea kushika bango sakata la Tundu Lissu kwa kuhamasisha wananchi kwenye mitandao ya kijamii kuweza kuchangua gharama za matibabu ili Tundu Lissu aweze kupatiwa matibabu hospitali mahiri duniani Lazaro Nyalandu amezidi kuwaomba Watanzania wote kumkumbuka Mbunge huyo kwa sala na dua wakati huu ambao amepata majaribu hayo na kuendelea kuwasisitiza kuchangia fedha kwa ili mbunge huyo apatiwe matibabu bora zaidi. "Tunawaomba wana Singida na Watanzania wote tuendelee kuchangia gharama za matibabu ya Mhe. Tundu Lissu sote tumkumbuke katika sala na dua zetu katika majira ya saa hii ya kujaribiwa kwake. Mungu akisema ndio, hakuna awezaye kupinga. Kwa wote wanaohusika moja kwa moja kumtibu na kumtunza, mikozo yao na fahamu zao zikahuishwe katika ubora wote wa utabibu na matunzo" alisema Nyalandu Aidha Mbunge huyo aliendelea kusema kuwa anaomba mazungumzo yanayoendelea na madaktari bingwa na hospitali mahiri yak...

Askari Aliyejifanya Faru John Ajisalimisha Kwa Mambosasa

Image
Askari anayejiita Faru John ameripoti Kituo Kikuu cha Polisi cha Kanda Maalumu ya Dar es Salaam alikohojiwa na kuruhusiwa kuondoka akaendelee na kazi. Kuripoti kwa askari huyo kunatokana na agizo alilolitoa jana Jumapili, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa kwa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Peter Sima awe amempeleka leo Jumatatu baada ya kutuhumiwa na wananchi wa Mbagala kwamba amekuwa akidai rushwa. Kamanda Mambosasa pia ametoa wiki moja kwa Kaimu Kamanda Sima awe amefuatilia tuhuma za rushwa zilizowasilishwa kwake na wananchi. Amesema askari huyo ataendelea kufuatiliwa ili kubaini ukweli wa tuhuma zilizotolewa dhidi yake na endapo zitathibitishwa taarifa zitawasilishwa kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi, Simon Sirro na atachukuliwa hatua za kisheria. “Kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Temeke alimleta huyu askari ambaye nimemuhoji na kumruhusu kuendelea na kazi wakati akiendelea kuchunguzwa ndani ya wiki moja,” amesema Kamanda Mambosasa. Akizungumza na wakaz...

Mwadui Watupia Lawama Nyasi Bandia Wasema Ndo Chanzo Cha Kushindwa Mchezo Wao Dhidi ya Simba

Image
Kiungo wa Mwadui, Awadh Juma amesema nyasi bandia zilikuwa kikwazo kwao jana kwenye mchezo wao dhidi ya Simba na hivyo kusababisha baadhi ya wachezaji kupata majeraha. Wachezaji watatu wa Mwadui akiwemo Awadh na Radhack Khalfan walishindwa kuendelea na mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru kutokana na  kupata majeraha. Awadh "Nilishindwa kuendelea na mchezo kwa sababu niliumia  misuli na hiyo yote kwa kwa sababu ya nyasi bandia. Tangu tumekuja tumefanya mazoezi siku moja tu kwenye uwanja huo  na jambo hilo limetugharimu na kusababisha wachezaji watatu kuumia. Hata hivyo Awad hakusita kukiri kuwa makosa waliyoyafanya ndio yaliyowapa Simba ushindi kutokana na wapinzani wao kutengeneza nafasi nyingi na kuzitumia. "Wapinzani wetu walitengeneza nafasi nyingi na kuzitumia lakini sisi  hatukutumia hata nafasi chache tulizopata. Tutayafanyia kazi makosa yote yaliyojitokeza ili kuhakikisha tunafanya vizuri katika michezo ijayo," alisema Awadh. T...

Nimepata Taarifa Polisi Wananitafuta...Sihitaji Kuviziwa - Peter Msigwa

Image
Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa amepata taarifa jeshi la polisi linamtafuta na kusema endapo jeshi la polisi litamwita kwa kufuata utaratibu basi na yeye ataitika wito huo ila si kuviziwa Mbunge Peter Msigwa akiwa na Mbunge Godbless Lema jana walipokwenda kwenye maombi katika kanisa la Lutheran Highway Nairobi! Mbunge Msigwa ametoa taarifa hii kufuatia kuwepo kwa taarifa toka jana kuwa kiongozi huyo naye anatafutwa na jeshi la polisi akidai kuwa ni moja kati ya watu waliokuwa wakiratibu mkusanyiko wa maombi ambao ulitakiwa kufanyika jana kumuombea Mbunge Tundu Lissu katika viwanja vya TIP Sinza jambo ambalo yeye mwenyewe alipinga na kusema bado yupo nchini Kenya. "Nimepata taarifa Kuwa polisi wamenitafuta toka asubuhi (jana) maeneo ya sinza, Wakisisitiza kuwa nipo hotelini hapo , wakati mimi niko Nairobi, nitaitika wito wa polisi ukiletwa rasmi, sihitaji kuviziwa +255754360996 mnaweza kunipigia au kuni...

Barnaba afunguka jinsi anavyo mmisi mama mtoto wake

Image
Mwalimu na mwanamuziki wa bongo Fleva, Barnaba Elias 'Barnaba Classic' amefunguka na kudai anam-miss sana mama Steve 'Zuu Namela' japokuwa kwa sasa hayupo tayari kumrudia mzazi mwenzake huyo. Msanii Barnaba akiwa na mama Steve 'Zuu Namela' enzi hizo mapenzi yakiwa moto moto kabla ya kuachana kwao. Barnaba ameeleza hayo baada ya kupita muda mrefu tokea aachane na mzazi mwenzake huyo na kupelekea kuwa single mpaka kipindi hiki. "Sitaweza kurudiana na mama watoto wangu japo nam-miss sana", amesema Barnaba. Aidha, Barnaba amesema kwa upande wake mapenzi hayajawahi kumuendesha hata kidogo kama baadhi ya watu wengine wanavyokuwa baada ya kuachana na wapenzi wao kwa kushindwa hata kuendelea kufanya kazi zao. "Niwe mkweli tu, mimi sijawahi kuendeshwa na mapenzi au mahusiano. Mapenzi hayana nafasi kubwa katika maisha yangu japokuwa yana nguvu kwa mtu yeyote yule, mapenzi hayajawahi kuchukua asilimia kubwa ya maisha yangu, kuniathiri wala...

Spika Ndugai: "Zitto hawezi kupambana na mimi"

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai, amesema ana uwezo wa kumzuia Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe kuzungumza mpaka mwisho wa bunge, kwani hawezi kupambana naye. Spika Ndugai ametoa kauli hiyo Bungeni ambapo amesema Zitto Kabwe hawezi na hapaswi kujibizana naye, na kumtaka Zitto Kabwe kutomfananisha na aliyekuwa Spika wa Bunge marehemu Samuel Sitta, kwani hawezi kufanana naye na kila mtu ana muda wake, kama ambavyo Spika wa bunge aliyepita mama Anna Makinda alivyokuwa na muda wake kuliongoza bunge hilo. Hapo jana Spika Ndugai alimtaka Zitto Kabwe kufika kwenye kamati ya maadili kutoa maelezo juu ya taarifa alizoziweka kwenye mtandao, na Zitto Kabwe kumjibu kuwa mambo anayoyafanya Spika yanaporomosha bunge