Posts

Showing posts from August, 2017

Mkuu wa Mkoa wa Zanzibar Awapost Ali Kiba na Diamond Awapa Ushauri Huu

Image
Wakati kukiwa bado fukuto kwa mashabiki mitaani kuhusu ni Ngoma ya Nani kali kati ya Aliyoachia Alikiba 'Seduce Me' na Zilipendwa ya WCB, basi hata serikalini wasanii hao wameendelea kugawagawa viongozi, ambapo Imeonekana Posti hii ya Diamond na Alikiba kwenye ukurasa wa Instagram wa mkuu wa mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mahmoud iliyoambatana na ujumbe huu "Nimeuelewa sana wimbo wa vijana wetu #wcb wakiongozwa na ndugu @diamondplatnumz hakika nimewaelewa sana kwenye wimbo wao wa #ZILIPENDWA, hii na pia nathamini kazi kubwa iliofanywa na kijana wetu ndugu yangu @officialalikiba, hakika wimbo wako ni wimbo nilio tokea kukubali. kama kiongozi niko proud sana na kazi nzuri zinazofanywa na vijana wetu kwa kutuwakilisha vyema nje ya mipaka yetu Ushauri wangu kwenu ni kua,tofauti zenu ziwe za kibiashara na sio vyenginevyo, #seduceme #fire#song #teammzikimzuri" Aliandika RC Ayoub

Mke wa Roma: Kama Roma Akitaka Kumuoa Mange Sina Shida Amuoe Tu

Image
Kwenye mitandao ya kijamii August 30, 2017 gumzo lilikuwa post ya mke wa Roma Mkatoli, Mama Ivan kwenye Instagram yake baada ya kuelezea kipande cha wimbo mpya wa Roma ‘Zimbabwe’ akisema kila anapokisikia hupata wivu. Licha ya kudai kuwandika maneno hayo kama utani huku wengi wakiyachukulia serious hadi kupelekea Mange Kimambi kuyanasa na kisha kuya post kwenye Istagram na kumuomba Mke wa Roma amruhusu awe mke mwenza ili amsaidie kumlinda Roma asiibiwe na wanawake wangine. Mke aliandika Instagram...“Kiukweli kila nikisikiaga huu msatari napata sanaaa wivu, utani utani hivi hivi mwisho wa siku inakuwa kweli, mimi mwenyewe alinianza kiutani utani hivi hivi, yani nyie!! wanaume hawa!! Kuolewa na msanii kunahitaji moyo” – Mke wa Roma Mke wa Roma alihojiwa na kufunguka akisema hakuwa serious bali kama Roma ataamua kumuowa Mange hatakuwa na usemi kwa kuwa mwanaume ndio mwenye maamuzi ingawa amedai hategemei kuona akioa mke mwingine kwa sababu dini hairihusu.

Ridhiwani amuandikia Dr. Kigwangalla ‘unaweza kuwa sehemu ya wachochezi”

Image
Mbunge kutoka Nzega vijijini ambae pia ni Naibu Waziri wa Afya Dr. Hamisi Kigwangalla na Mbunge Chalinze Ridhiwani Kikwete kwenye hii post ambapo ishu imeanzia kwenye alichopost Dr. Kigwangalla. Aliweka picha ya vijana wa Kitanzania wakionekana kupambania kupata kazi TRA ambapo iliripotiwa kwamba nafasi za kazi zilizotangazwa na TRA ni 400 lakini waliojitokeza ni zaidi ya elfu 30. Sasa baada ya kuiweka hiyi picha Dr. Kigwangalla aliandika “ Je, hii inaashiria ukubwa wa tatizo la ajira nchini ama ni kwamba watu wetu wanachagua sana kazi za kwenda? #NjeyaBox” Baada ya picha hiyo kupostiwa kwenye Twitter ya Dr. Kigwangalla baadhi ya Watanzania walitoa maoni yao ambapo miongoni mwao ni Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete aliemuandikia >>> “ Unaweza dhani unauliza swali kumbe nawe unakua sehemu ya wachochezi! Mh. Waziri unaweza kuwa hujui kusoma lkn picha inatoa jibu sahihi”

Manji Ashindwa Kufika Mahakamani Kujitetea Kutokana na Tatizo la Kiafya

Image
Mfanyabiashara Yusuf Manji ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 31, 2017 kujitetea katika kesi inayomkabili ya dawa za kulevya kutokana na sababu za afya. Hayo yamesemwa mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha baada ya Wakili wa Serikali Mkuu, Timony Vitalis kwamba kesi hiyo inaendelea na ushahidi. Hata hivyo, kesi hiyo haikuweza kuendelea baada ya kutolewa taarifa ya Magereza kwamba Yusuf Manji anaumwa na amepewa mapumziko ya kitanda. Baada ya kuelezwa hayo, kesi imeahirishwa hadi September 18, 2017.

Upande wa Utetezi Umeeleza Sethi Amewekwa Puto Tumboni Kutokana na Matatizo ya Kiafya

Image
Upande wa utetezi umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Mmiliki wa Kampuni ya kufua umeme ya IPTL, Harbinder Singh Sethi amewekewa ‘Puto’ tumboni kutokana na ugonjwa unaomkabili hivyo asipohudumiwa inavyotakiwa anaweza kupoteza maisha. Mbali ya Seth, mwingine ni Mfanyabiashara James Rugemarila ambapo kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 12, yakiwemo ya kutakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya TSh 309,461,300,158. Wakili wa utetezi, Joseph Mwakandege amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi kuwa mteja wake Seth anatakiwa apelekwe Hospital ya Taifa Muhimbili lakini hadi sasa hajapelekwa na ni dhahiri upande wa mashtaka umedharau amri mbili za Mahakama. ”Ugonjwa uliosababisha Seth atakiwe kwenda Muhimbili ni baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa ambapo tumboni kwake kumewekwa Balloon ‘Puto’ hivyo asipohudumiwa ipasavyo inaweza kusababisha kifo, naomba mshtakiwa apelekwe Muhimbili kwa sababu ni Hospitali ya juu na yenye vifaa na watalaamu wa kutosha“ ...

Pamoja na Umaarufu Alio nao ALIKIBA Kwa Nini Bado Maskini na Diamond Platnumz ni Mwanamuziki Tajiri?

Image
Naombeni uzii huu usichukuliwe kiushabiki bali uchukuliwe kama haki ya kila mtu kutoa ya moyoni pasipo kuvunja sheria Kwa mda mrefu msanii Alikiba amekuwa yupo kwenye game la mziki na amejizolea umaarufu mkubwa kwa kazi zake nzuri na kujipatia mashabiki wengi huku wengine wakimuita "KING" wa bongofleva. Lakini pamoja na umaarufu wake alionao na mashabiki wengi aliojizolea lakini bado Alikiba ni mtu mwenye maisha ya ya chini tu ambayo hayafanani kabisa na umaarufu wake Tukija upande wa pili wa mwanamuziki Naseeb Abdul ~Diamond Platnumz yeye si wazamani sana kwenye game kama alikiba lakini nayeye ametokea kufanya kazi nzuri na kujizolea mashabiki wengi na umaarufu lakini hajaweza kufikia record ya The king himself Alikiba Lakini ukija kwenye maswala ya maendeleo ambayo ndio kipimo cha kazi anayofanya msanii utagundua kuwa Diamond platnumz amejizolea utajiri wa kutisha zaidi ya King himself Alikiba. Kutokana na kazi ya mziki Diamond platnumz ameweza kujipatia...

MAHAKAMANI: Agnes Masogange anayo kesi ya kujibu

Image
Mwingine ambae alifika Mahakamani leo kuendelea kufatilia kesi yake ni Video Queen Agnes Gerald ‘masogange’ ambapo kesi yake ni kuhusu tuhuma za utumiaji wa dawa za kulevya. Habari mpya ya leo kuhusu kesi hiyo ni kwamba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imesema Agnes anayo kesi ya kujibu katika kesi ya kutumia dawa za kulevya hivyo anapaswa kujitetea. Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri amesema kuwa amekubaliana na hoja za ushahidi wa upande wa mashtaka ambapo mshtakiwa amekutwa na kesi ya kujibu na ana haki ya kujitetea . Baada ya kuelezwa hayo, Masogange amesema atajitetea kwa njia ya kiapo na atakuwa na mashahidi watatu ambapo kesi imeahirishwa hadi October 12, 2017 ambapo Agnes ataanza kujitetea.

KAZI IMEANZA DSM: Kamanda mpya kaongea tena leo

Image
Tunae Mkuu mpya wa Polisi kwenye kanda maalum ya kipolisi ya Dar es salaam Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Lazaro Mambosasa ambae amechukua nafasi ya Simon Sirro ambae kwa sasa ndio Mkuu wa jeshi la Polisi Tanzania. Jumla ya Majambazi wanne kati ya 6 wamejeruhiwa kwa risasi na Polisi na kukamatwa kwenye eneo la Kigogo Dar es salaam baada ya mpango wao wa kwenda kuvamia kugundulika na Polisi kuwawekea mtego, majeruhi walipelekwa Muhimbili Hospital na baadae kufariki. Polisi Dar es salaam pia imefanya oparesheni na kuwakamata watu 193 kwa makosa mbalimbali ya kihalifu ikiwemo wacheza kamari, utapeli, bangi na mengine…

Mzee wa Kimasai mwenye Wake 8 na Watoto 70 akawajengea na shule kabisa ili wasipate tabu

Image
Umeshawahi kujiuliza kama itatokea siku moja utakua na Watoto wengi kiasi kwamba itakubidi uwajengee Shule yao wenyewe sababu wako wengi na haiwezekani kuwapeleka kwenye shule nyingine sababu ziko mbali? hii imetokea Arusha. Mzee Laiboni ana umri zaidi ya miaka 100 ambapo katika maisha yake, idadi ya Wake aliwaoa ni 8 aliamua kuanzisha shule yake kwa ajili ya Watoto wake na Wajukuu baada ya mtoto mmoja kugongwa na gari siku moja akienda shule hivyo akaamua kujenga shule karibu na nyumbani.

Simba sasa kumburuza Buswita mahakamani Thursday, August 31, 2017

Image
MKUU WA IDARA YA HABARI NA MAWASILIANO WA SIMBA, HAJI MANARA. LICHA ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kumfungia kiungo wa Mbao FC, Pius Buswita, kutocheza soka kwa kipindi cha mwaka mmoja kutokana na kusaini kuzichezea klabu mbili tofauti, Simba na Yanga, sasa ataburuzwa mahakamani, imeelezwa. Klabu ya soka ya Simba, imesema inatarajia kumfikisha mahakamani Buswita, kwa madai kuwa amewatapeli fedha zao wakati akijua alishasajiliwa na Yanga.

Hali tete:Chadema yatangaza mgogoro na serikali

Image
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza mgogoro na mkuu wa wilaya ya Momba, Juma Irando kwa kuagiza jeshi la polisi wilayani humo kumuweka ndani kwa saa 48 mbunge wa Jimbo la Tunduma, Frank Mwakajoka kwa madai ya uchochezi. Katika kikao alichofanya na wanahabari, Mwenyekiti wa CHADEMA, Halmashauri ya mji wa Tunduma, Ali Mwafongo ameleezea kusikitishwa na amri hiyo ya mkuu wa wilaya na kusema kuwa kamwe hawatarudi nyuma huku akiahidi kutompa ushirikiano mkuu wa wilaya huyo. "Uchungu tunaopata sasa hivi tunajua ipo siku itakuwa furaha kwetu kwani ushindi unakaribia. Kinachofanywa sasa hivi wakumbuke ipo siku watawala watakuwa wapinzani na haya yanayofanywa hayataweza kuturudisha sisi nyuma. Viongozi wetu wamekuwa wakipelekeshwa sana lakini katu hatutokata tamaa kwa sababu ni kazi yetu kusema ukweli na kuwatumikia wananchi wetu" alisema Mbali na hayo mkuu huyo wa wilaya pia ametuhumiwa kutoa amri ya kushusha bendera za chama hicho hali ambayo im...

Dkt. Makongoro Mahanga Akamatwa na Kufikishwa Mahakamani

Image
Mbunge wa zamani wa Ukonga na Segerea, Dk Makongoro Mahanga amekamatwa na Polisi Mkoa wa Ilala kwa amri ya Mahakama Kuu na amefikishwa mahakamani. Mahakama iliamuru Dk Mahanga akamatwe na kufikishwa mahakamani kwa kushindwa kutekeleza uamuzi unaomtaka amlipe mdai Kainerugaba Msemakweli Sh14 milioni. Fedha hizo ni gharama za kesi alizozitumia Msemakweli baada ya kushinda kesi ya madai ya kashfa ambayo Dk Mahanga alimfungulia kwa kumtaja kwenye kitabu chake kinachoitwa: “Mafisadi wa Elimu”. Katika kitabu hicho anamtaja kuwa ni mmoja wa viongozi wenye shahada za udaktari wa kughushi. Kati ya kiwango hicho cha fedha, Dk Mahanga ameshalipa Sh6 milioni hivyo anadaiwa Sh8 milioni.

Huu ndio wimbo wa kwanza utakao toka katika studio ya Rayvan

Image
Je unaufahamu wimbo wa kwanza ambao utaanza kutoka chini ya studio mpya ya Rayvanny, Surprise Music? Basi fahamu kuwa ngoma iitwayo ‘Ngarenaro’ ya Dogo Janja unaotarajiwa kutoka rasmi Jumatano hii ndio utakuwa wa kwanza kutoka chini ya studio hiyo ambapo Rash Don ndio mtayarishaji wake. Hata hivyo tayari kuna wasanii wengine wakubwa wanadaiwa tayari wameshafanya ngoma katika studio hiyo akiwemo Madee, Maromboso na wengine.

Gwiji wa Barcelona ashinda bahati nasibu Qatar

Image
  Kiungo Xavi Hernandez ameshinda bahati nasibu ya benki nchini Qatar. Kwa sasa, Xavi anakipiga katika timu maarufu nchini Qatar ya Al Saad. Xavi ambaye ni gwiji la Barcelona anayekipiga nchini humo, alishinda  euro 229,000 baada ya kufungua akaunti katika benki ya Doha. Benki hiyo ilikuwa ikiendesha bahati nasibu kwa wateja wake wote waliofungua akaunti.

safari ya oxlade Chamberlain kwenda liverpool yaiva

Image
Liverpool wameanza mazungumzo na Arsenal kuhusu uhamisho wa kiungo wa kati Alex Oxlade-Chamberlain. Mchezaji huyo wa miaka 24 alikataa kuhamia Chelsea Jumanne hata baada ya klabu hizo kuafikiana kuhusu uhamisho wake wa £40m. Oxlade-Chamberlain anayechezea timu ya taifa ya England anataka kucheza kama kiungo katika safu ya kati na anahisi kwamba anaweza akapata nafasi Anfield. Alikataa kuhamia Chelsea baada ya kugundua kwamba huenda wakataka kumtumia katika upande wa kushoto uwanjani. Bado haijabainika iwapo Liverpool watafikia dau ambayo Chelsea walikuwa wamewasilisha. Oxlade-Chamberlain anatumikia mkataba wake wa mwisho Emirates na amechezea mechi zote nne za Arsenal msimu huu licha yake kumwambia meneja Arsene Wenger kwamba hatatia saini mkataba mpya. Alishangiliwa na wachezaji wa Liverpool alipoondolewa uwanjani wakati wa mechi ya Jumapili ambayo Arsenal walilazwa 4-0 uwanjani Anfield Jumapili. Kiungo huyo wa kati amechezea Arsenal mechi 198 tangu ajiunge nao ku...

Yemen:Idadi ya waliokufa na mafuriko yaongezeka

Image
Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali kusini mwa Yemen yamesababisha vifo mpaka kufikia watu 14 sasa. Kwa mujibu wa habari,watoto wadogo pamoja na wanawake ni kati ya wale waliopoteza maisha katika mafuriko yaliyotokea Lahij nchini Yemen. Barabara zimefungwa kukabiliana na mafuriko nchini humo. Ripoti zinaonyesha kuwa mvua kubwa kama hiyo haijanyesha nchini humo kwa miaka 15 sasa. Facebook Twitter Google+ Pinterest Linkedin

Dkt. Mwakyembe awaasa vijana kuwa hamna uchawi kwenye michezo

Image
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amewaasa na kuwataka vijana kutumia nguvu zao katika michezo na kufanya mazoezi ila wasije kufikilia kama kuna njia za mkato wala uchawi bali mazoezi ndiyo kila kitu. Dkt. Mwakyembe amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa bendera ya Taifa mbele ya waandishi wa habari na vijana waliyorejea kushiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo Afrika Mashariki (FEASSSA) yaliyofanyika mwaka huu katika Mji wa Gulu Nchini Uganda  ambayo hushirikisha timu za shule za sekondari za jumuiya ya Afrika Mashariki. "Nataka kuwadhitibishia Watanzania kwamba tutaenzi daima michezo ya UMITASHUMTA na UMISETA maana vipaji ndiyo vinapoanzia, niwapongeze sana vijana kwa kushinda medali nIwatie moyo muendelee ili muweze kushiriki katika mashindano ya kimataifa yakiwemo Olimpiki, maana nyinyi ndiyo warithi wa Simbu na wanariadha wengine waliowahi kufanya vyema hapa nchini," alisema Dkt. Mwakyembe...

Alikiba, Diamond, Lulu na Millard ayo watajwa 100 bora ya Vijana Afrika

Image
Tuzo za VIJANA 100 WA AFRIKA wenye ushawishi mkubwa kwa jamii kwa mwaka 2017 zimeiachia orodha ya vijana wa mataifa mbalimbali waliochaguliwa kuwania ambapo orodha inaendelea kutajwa na mpaka sasa Watanzania watano wametajwa. Watanzania hao ni Waimbaji Alikiba , Diamond Platnumz , Mwanamitindo Flaviana Matata na Mwigizaji Lulu na Millard Ayo wengine ambao wametajwa tayari wanatokea kwenye mataifa ya  South Africa , Libya , Ghana  na  Nigeria .      

Ni kweli fuvu limefukuliwa uwanja wa Taifa? ukweli huu hapa

Image
Baada ya taarifa kusambaa katika mitandao ya kijamii na picha zikisambaa kutoka uwanja wa Taifa kwa madai kuwa, kipindi hiki ukarabati wa uwanja huo sehemu ya pitch imeonekana fuvu la kichwa cha mtu, taarifa ambazo zimesambaa sana katika mitandao ya kijamii. Imaniabel.blogsport.com ikalazimika kufuatilia kwa kina kuhusiana na stori hizo kwa mkurugenzi msaidizi wa idara ya michezo Alex Nkenyenge ili atoe taarifa kamili kuhusiana na tetesi zilizokuwa zinasambaa ni kweli ni fuvu? Kwanza hiyo ni taarifa ya uongo na hakuna fuvu isipokuwa ni madude ambayo yamepatikana kwenye mchanga baada ya kuwa tumefukua sehemu ya uwanja, kwa hiyo hakuna kitu kinachoitwa fuvu la mtu wala nini ni madude tu yaani mamimea yale yaliyooza basi yanafanana kama magimbi ambapo ndani lilikuwa limeshaliwa” “Sasa kwa sababu mtu analiona kwa mbali anasema fuvu sasa sijui fuvu litakujaje hapa, kwanza kilichotokea hilo dude limekuja na mchanga wala halikuwa ndani ya uwanja, yaani kwenye mchanga uliyol...

Aliche kisema Ally Kiba baada ya kutajwa katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika

Image
Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Alikiba kutajwa kuingia katika orodha ya vijana 100 wenye ushawishi Afrika 2017, ameelezea furaha yake. “Najisikia vizuri kwamba Africa nzima imekutambua, kuna watu ambao wanatamani kuwa kama Alikiba na vitu kama hivyo. Kwa hivyo nawahamasisha vijana wengine kufanya kazi nzuri kama mimi nivyofanya, nashukuru sana, najisikia vizuri,” ameiambia The Playlist ya Times Fm. Vijana wengine wa kitanzania waliotajwa katika orodha hiyo iliyotolewa na African Youth Awards  ni pamoja na Nancy Sumari, Diamond Platnumz, Elizabeth ‘Lulu’ Michael, Flaviana Matata, Millard Ayo na Jokate

HESLB yaongeza muda wa uombaji mikopo vyuo vikuu

Image
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongeza muda wa wanafunzi kuwasilisha maombi ya mikopo. Hatua hiyo imeelezwa inalenga kutoa nafasi kwa wanafunzi walioshindwa kufuata masharti kuyakamilisha. Mkurugenzi Mkuu wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru amesema muda huo umeongezwa hadi Septemba 11 badala ya Septemba 4. “Tumesogeza mbele kwa siku saba zaidi ili walioshindwa kufuata vigezo wakati wa kujaza fomu wafanye hivyo,” amesema. Amesema hadi kufikia jana Agosti 29, wanafunzi waliojitokeza walikuwa 49,282 lakini ni 15,473 waliokamilisha maombi kwa njia ya mtandao.

Rais Magufuli Asitisha Bomoa bomoa Dsm

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe, Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda WAMESITISHA zoezi la BOMOA BOMOA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba (17, 000) zilizotangazwa KUBOMOLEWA na Baraza la Hifadhi ya Mazingira NEMC. Hatua ya kusitisha zoezi hilo, Imekuja kufuatia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Paul Makonda KUZUNGUMZA na Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli kuhusiana na Sintofahamu ya bomoa bomoa hiyo ambayo AMEMUELEZA Mhe Rais Magufuli kuwa Taarifa za BOMOA BOMOA ya Nyumba elfu kumi na saba iliyotolewa HAIKUFIKA ofisini Kwake Jambo ambalo ni tofauti na Taratibu za Utendaji kazi wa Serikali.  Kutokana na Sababu hizo, Mhe Makonda amesema Mhe Rais amesikitishwa na TAMKO hilo la kutaka KUBOMOLEWA kwa Nyumba zaidi ya elfu kumi na saba na ametoa pole kwa Wananchi waliokumbwa na TAHARUKI ya TAMKO hilo la Ubomoaji, na kusisitiza kuwa Mhe Rais, Dkt. John Pombe Magufuli HAKUCHAGULIWA kwa ajili ya KUBOMOA Nyumba ...

Moyo wa Yusuph Manji Wawekewa Vyuma Ili Kumsaidia Kupumua

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKIC), Prof. Mohammed Janab ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 30, 2017 kuwa moyo wa Mfanyiabiashara Yusuf Manji umewekwa vyuma ili kumsaidia kupumua. Prof. Janab ambaye ni Daktari wa moyo na Shahidi wa kwanza upande wa uetetezi ameyasema hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati akitoa ushahidi katika kesi ya dawa za kulevya inayomkabili Manji ambapo akiongozwa na Wakili wa utetezi, Hajra Mungula, alisema yeye ni Daktari wa moyo wa Taasisi ya JKIC. Amesema anamfahamu Manji baada ya kufikishwa katika Taasisi hiyo February 2017 akiwa mwenye matatizo ya moyo na kuongeza kuwa alipofikishwa hapo alifanyiwa vipimo na jopo la madaktari lililobaini Moyo wake umewekewa vyuma ambapo akaingizwa mipira maalum na kubaini kwamba upo katika hali nzuri. ”July 2017 alirudishwa tena katika Taasisi yetu akiwa na tatizo hilo la moyo pamoja na maumivu ya mgongo na kutokuwa na usingizi.” Prof...

Aunty Afunguka Sababu Ya Kuhudhulia Uzinduzi wa Filamu ya Wema Bila Iyobo

Image
    Mrs Iyobo kwa sasa Aunty Ezekiel, ameamua kutoa ufafanuzi wa kutinga peke yake katika usiku wa kuitazama filamu mpya ya shoga yake Wema Sepetu iitwayo ‘Heaven Sent’. Akiongea na Bongo5, mrembo huyo ambaye amejulikana kupitia filamu ameeleza kuwa hakufika na waubani wake, Moses Iyobo kutokana na mtoto wake Cookeis kuugua. “Moses hajaja kwa sababu mtoto alikuwa hayupo sawa, so nikaona sio vizuri wote tukija huku na nikisema mimi nibaki. Wema she is my friend so inakuwa sio vizuri, nikasme awacha mie nije ye abaki,” amesema mrembo huyo. Filamu ya Heaven Sent ilizinduliwa kwa mara ya kwanza siku ya Jumamosi na mastaa kibao wahudhuria uzinduzi huo akiwema Elizabeth Michael ‘Lulu’ na Steve Nyerere.

Msuva Anatarajiwa Kuwasili Usiku wa Leo

Image
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Difaa EL Jadida,  Simon Msuva anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo (Jumanne) kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Botswana. Msuva ni miongoni mwa wachezaji saba wanaocheza nje walioitwa na Kocha Salum Mayanga kwa ajili ya mchezo huo wa Septemba 2 utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru. Leo mchana kwa saa za Morocco, Msuva ataiongoza Al Jadida kuivaa FUS Rabat katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini 'Botola Pro League. Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema mchezaji huyo ataungana na wenzake ambao wameshaanza maandalizi ya mchezo huo. "Wachezaji wa ndani wapo na Mbwana Samatta pia amewasili, leo usiku tunamtarajia Msuva kutoka Morocco," alisema Lucas. Wachezaji wengine wanaocheza soka nje waliotwaa ni pamoja na Orgenes Mollel anayecheza FC Famalicao, Ureno na kiungo wa Sony Sugar ya Kenya, Hamis Abdallah.    

Hii Hapa Picha Iliyomsababisha Young Dee Kuomba Radhi Mashabiki

Image
nasemekana Rapa Young Dee na Amber Lulu wanajipanga kutoa ngoma yao pamoja baada ya picha ya kimahaba yenye utata mwingi kuachiwa leo mitandaoni. Picha hii inamuonyesha Young Dee akiwa anashanga makalio ya Amber Lulu, Ni miongoni mwa picha zitakazotoka katika photoShoot ya kazi yao mpya.

Justin Bieber Swollen Balls Triggers Hospital Lawsuit

Image
  Justin bieber  went to the ER back in May fearing a soccer injury had caused one of his testicles to twist, and that triggered a nasty legal claim between the hospital and a fired employee. Justin made an emergency run to Northwell Health in Long Island New York, and a staffer named Kelly Lombardo found out about it. The hospital claims Lombardo illegally accessed Justin's medical file in one of the computers ... this after hearing rumors Justin had been admitted for an STD. According to the lawsuit, the hospital fired Lombardo for being "an immoral employee" who violated Bieber's privacy rights. Lombardo has just filed a wrongful termination lawsuit, claiming she never accessed Justin's file and simply heard from others he was there for treatment of an STD. Sources connected to Justin tell TMZ, he did NOT go to the hospital for an STD. They say he had been playing soccer and suffered a painful injury. Justin "WebMD'd himself" in...

The Kardashians We're Giving $500k For Harvey Relief

Image
The Kardashains have stepped up to the plate in a huge way to help the victims of Hurricane Harvey. Sources with direct knowledge of the situation tell us Kim , Kris , Khloe , Kendall , Kylie and Kourtney gave $500,000 to The Red Cross and The Salvation Army Tuesday. We're told the money will be wired and will be split evenly. The Kardashians were touched by the courage and bravery of those in Houston battling the storm and those helping with relief efforts. The donation is one of a number made by celebs since Kevin Hart started a movement Monday challenging other Hollywood heavyweights to pitch in.

Maria Sharapova Grand Slam return at the US open 2017

Image
Former world number one Maria Sharapova made a triumphant return to Grand Slam competition Monday after a 15-month doping ban, outlasting second-ranked Simona Halep 6-4, 4-6, 6-3 at the US Open. The 30-year-old Russian, who had only one hard court tuneup match due to a nagging forearm injury, swatted 60 winners with 64 unforced errors, setting the tempo and baffling Halep at times in a tension-packed thriller at Arthur Ashe Stadium. “This girl has a lot of grit,” Sharapova said of herself. “And she’s not going anywhere.” Sharapova, who tested positive for meldonium at last year’s Australian Open, improved to 7-0 in her all-time rivalry with Halep, extending her mastery over the 25-year-old Romanian. “I just thought this was another day, another opportunity, another match but this was so much more,” Sharapova said. “You sometimes wonder why you put in all the work and this is exactly why.”An emotional Sharapova punctuated her sho-tmaking, at times erratic and other ...

Cheka, Miyeyusho wafungiwa na TPBC, faini juu

Image
Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (TPBC) limewafungia na kuwapiga faini ya Tsh. 200,000/ mabondia Cosmas Cheka na Francis Miyeyusho wakidaiwa kufanya vurugu baada ya kushindwa katika mapambano yao. Shirikisho hilo limechukua hatua hizo kutokana na fujo zilizotokea usiku wa kuamkia jumapili katika michezo iliyofanyika ukumbi wa Vijana Social hall Kinondoni Dar es salaam. Kutokana na kitendo hicho kamisheni imewaonya Bondia wote watakao jihusisha na vitendo vya uvunjifu wa amani wakati wa michezo mahali popote kuwa watachukuliwa hatua kali za kinidhamu ikiwemo kulipa faini. Hata hivyo TPBC imewaomba radhi kwa fujo zilizotokea na kuwaahidi kutotokea tena mahali popote. Adhabu za mabondio hao zinatarajia kuanza kutekelezwa Septemba 5 mwaka huu.

Simba kukabidhiwa Ngao ya Jamii mbele ya Azam FC

Image
Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) limerekebisha Ngao ya Jamii upya kwa ajili ya klabu ya Simba baada ya ile ya awali kukosewa kuandikwa baadhi ya maneno. Mabadiliko hayo yamefanyika baada ya makosa yaliyofanyika Agosti 23 mwaka huu ya kimaandishi kwenye Ngao ya Jamii ambapo Simba waliibuka washindi na kukabidhiwa Ngao hiyo. Ngao ya Jamii iliyotolewa kwa Simba iliandikwa ‘Community Sheild’ badala ya ‘Community Shield’ kitu ambacho kilizua mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea (TFF) kuomba radhi kwa wanafamilia wa mpira wa miguu nchini na kuahidi tukio kama hilo halitojirudia tena. TFF kupitia afisa habari wake, Alfred Lucas ameionesha Ngao ya Jamii iliyofanyiwa marekebisho na kusema kuwa Ngao hiyo itakabidhiwa kwa Simba siku ya jumatano ya tarehe 6 Septemba kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Azam FC.

Aliyekuwa meneja wa Ommy Dimpoz afunguka haya

Image
MUBENGA aliyekuwa meneja wa msanii, Ommy Dimpoz, ameibuka na kusema kuwa tangu aache kumsimamia msanii huyo, amepoteza dira kimuziki, ndiyo maana hatoi nyimbo kwa wakati. “Tukizungumza kwa namna ambavyo mimi nimefanya kazi na Ommy, vitu vingi vinavyomtokea sasahivi sielewi hata mimi nashangaa, kwa sababu ukiangalia hata kwenye gemu yetu hafanyi vizuri tena, sijui anakosea wapi, hata kazi zake hazina ubora na hazitoki kwa wakati. “Nakumbuka wakati tunafanya kazi kuanzia Nai Nai, Baadaye, Ndagushima, Me and You, Tupogo, Wanjera ni nyimbo ambazo zilikuwa zinatoka kwa wakati, na mapokezi yake yalikuwa ni makubwa sana. “Sijui labda yeye mwenyewe anajiona wapi, lakini mimi simuoni pale ambapo nilikuwa nimemfikisha,” amesema Mubenga. Baada ya kutemana na Mubenga, Ommy Dimpoz kwa sasa yupo chini ya menejimenti ya Rockstar, ambayo ndiyo inayomsimamia Ali Kiba.  

Mbunge wa Tunduma atakiwa kukamatwa

Image
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Momba mkoani Songwe imeagiza kukamatwa mara moja kwa Mbunge wa Jimbo la Tunduma kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mh.Frank Mwakajoka kwa tuhuma za kuwadhihaki wateule wa Rais. Kamati ya Ulinzi na usalama wilayani ya Momba imeagiza kiongozi huyo kukamatwa baada ya kumdhihaki Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Mhe. Chiku Galawa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Momba Mhe. Juma Said Irando.

Msafara wa DC washambuliwa na watu wasiojulikana

Image
Karagwe. Msafara wa Mkuu wa Wilaya ya  Karagwe, Godfrey Mheluka uliokuwa katika operesheni ya kuwaondoa watu wanaodaiwa kuvamia maeneo ya wafugaji katika Kijiji cha Kashanda, Kata ya Nyakahanga, umeshambuliwa na watu wasiojulikana. Katika shambulizi hilo lililotokea leo Agosti 29 saa tano asubuhi, diwani wa Nyakahanga, Charles Bechumila amejeruhiwa na amepelekwa katika Hospitali Teule ya Nyakahanga. Mkuu wa wilaya hiyo, Mheluka amesema bado hajawa sawa, hivyo atazungumzia tukio hilo  baadaye. Ofisa Tarafa ya Bugene Nyaishozi, Rozaria Christian amesema walikuwa kwenye operesheni halali na wakulima hawana na taarifa. Amesema baada ya kuwakamata wawili ndipo kundi la watu lilijitokeza likionyesha kuwa lilijiandaa kuwashambulia. Christian amesema watu kadhaa wamekamatwa wakituhumiwa kuhusika kumjeruhi diwani huyo. Shuhuda wa tukio hilo aliyekuwa kwenye msafara huo amesema baada ya kufika kijijini humo aliwakuta baadhi ya watu wakilima na walikamatwa. Baada ya ...

Vita ya diamond na Ally kiba kuhamia tena AFRIMA

Image
Ni taarifa nzuri kwa muziki wa Tanzania baada ya Waandaaji wa All African Music Awards ‘AFRIMA’ wametangaza list ya wasanii wanaowania tuzo katika vipengele mbalimbali kwa mwaka 2017 ambazo hujumuisha Mastaa kibao katika tasnia ya muziki wa Afrika November 10-12, 2017. Kuna jumla ya wanamuziki 33 waliotajwa kuwania tuzo mbalimbali lakini wamegawanywa katika Kanda Tano ambazo ni Afrika ya Kati, Afrika Mashariki, Afrika Kusini, Afrika Kaskazini na Afrika Magharibi huku pia kukiwa na tuzo zinazojumuisha Afrika nzima. Muziki wa Bongofleva haujaachwa kwenye list hiyo ambapo mastaa kutoka Tanzania Diamond Platnumz, Alikiba, Darassa, Lady Jay Dee, Vanessa Mdee, Nandy, Feza, Msafiri Zawose na Topher Jaxx. Best Female Artiste Eastern Africa Artiste Track Country Chess Nthussi Give it to you Kenya Feza Walete Tanzania Juliana Kanyomozi I am Still Here Uganda Lady Jaydee Sawa Na Wao Tanzania Nandy One Day Tanzania Vanessa Mdee Cash Madame Tanzania Vi...